Juisi ya papai: Maandalizi na faida zake

Na Lucy Samson
17 Jan 2023
Juisi ya papai huimarisha kinga mwili, hupambana na visababishi vya saratani, huongeza uoni na kupunguza maumivu yatokanayo ya hedhi.
article
  • Juisi ya papai ni chanzo kizuri cha vitamini A, B29, C, madini chuma pamoja na nyuzi nyuzi. 
  • Inaimarisha kinga mwili, inapambana na visababishi vya saratani. 

Papai ni moja ya matunda yanayopatikana kwa wingi nchini Tanzania. Baadhi ya watu hupanda miche ya matunda hayo majubani hivyo kurahisisha upatikanaji wake.

Kwa miaka mingi tunda hili limekuwa likitumika kama tiba kwa mtu mwenye shida ya kupata choo (Constipation). Pia kama kiungo muhimu cha kulainisha nyama wakati wa mapishi.

Mbali na hayo tunda hilo pia lina wingi wa vitamini ikiwemo Vitamini A, B29, C, madini chuma pamoja na nyuzi nyuzi ambayo unaweza pia kuzipata kwenye juisi inayotokana na tunda hilo.

8 Amazing Benefits of Papaya for Health and Skin - NDTV Food
Mbali na faida nyingi za juisi hii, pia nikiburudisho kizuri wakati wa asubuhi, mchana au jioni. Picha | NDTV.

Kwa mujibu wa tovuti ya afya netmeds ya nchini India, juisi ya papai ina mchango mkubwa kwenye kuimarisha kinga mwili, kupambana na visababishi vya saratani, kuongeza uoni na kupunguza maumivu yatokanayo ya hedhi.

Ikiwa wewe ni  miongoni mwa wanaotamani kupata faida za juisi ya tunda hili basi ambatana nami kwenye makala hii tujifunze namna ya kuandaa ili ufaidike na faida nyingi kwenye mwili wa binadamu.

Maandalizi  

Hatua ya kwanza katika utengenezaji wa juisi ya papai ni kuliosha na kumenya maganda ya nje. 

Ukimaliza kumenya ligawe mara mbili na uondoe mbegu zote zilizopo katikati ya papai. Unaweza kuliosha tena kuhakikisha matunda yote ya katikati yametoka.

Andaa blenda ya kusaga na uweke vipande vya papai vilivyo katwakatwa kwa saizi ndogo. Ongeza sukari, maji au kikombe kimoja cha maziwa ikiwa unapendelea.

Papaya Coconut Smoothie - Recipe - nutribullet
Juisi ya papai inaweza kutengenezwa kwa kuongeza vipande vya nazi na kuongeza ladha na vitamini zaidi. Picha | Nutribullet

Ongeza maji ya ndimu kijiko kimoja kisha usage mpaka ilainike vizuri.

Haina haja ya kuchuja ikiwa umesaga kwa muda mrefu na kupata mchanganyiko mzito usio na mabonge mabonge.

Mpaka hapo juisi ya papai inakuwa tayari kwa kunywa. Unaweza kuongeza vipande vya barafu au kuweka kwenye jokofu kwa ajili ya matumizi ya baadaye. Unasubiri? Tengeneza leo!

© Copyright 2021 JikoPoint by Nukta Africa