Huu ndio utamu wa biskuti zilizotengezwa nyumbani

Na Fatuma Hussein
5 Mar 2024
Jikopoint imekuandalia maujanja ya kuandaa kitafunwa hiki nyumbani ili kuepuka gharama zisizo za lazima za kununua biskuti mara kwa mara.
article
  • Unaweza kutengeneza ladha unayotaka huku ukipunguza gharama za kununua kitafunwa hicho mara kwa mara.

Hakuna asiyefahamu utamu wa biskuti kunzia watoto, watu wazima hadi wazee.

Umaarufu wa kitafunwa hiki hautokani tu na ladha tamu iliyopo bali ni urahisi wake wa kupatikana katika maduka makubwa au hata yale madogo  yaliyopo mtaani.

Ili kufurahia utamu wa kitafunwa hiki bila kuingia gharama zisizo za lazima za kununua biskuti mara kwa mara Jikopoint imekuandalia maujanja ya kuandaa kitafunwa hiki nyumbani.

Mbali na kupunguza gharama unaweza kutumia ujuzi huu kutengeneza biskuti zinazoendana na mahitaji yako mathalan kwa wasiopenda sukari nyingi au ladha fulani ambazo huwekwa katika biskuti za viwandani.

Pia ujuzi wa kuandaa biskuti nyumbani unaweza kukusaidia kujiongezea kipato ambapo unaweza ukauza katika mgahawa, au eneo lolote unalopendelea.

Tuingie jikoni

Bila kupoteza muda tuanze mapishi yetu kwa kuandaa bakuli kubwa safi litakalotumika kuchanganyia mahitaji uliyonayo.

Anza kwa kuweka siagi (unaweza kutumia aina yoyote uliyonayo)  weka sukari na uichanganye vizuri, ongeza yai moja moja mpaka yote matatu 4 yatakapoisha huku ukiendelea kukokoroga.

Kama unapendelea ladha nyingine kama tangawizi huu ndio wakati wa kuweka,hakikisha unatumia kwa kwa kiasi ili isije ikaharibu biskuti yako.

Baada ya hapo weka ngano iliyochekechwa vizuri kisha uchanganye mpaka ilainike vizuri kwa dakika saba mpka 10.

Hakikisha mchanganyiko wako ni mgumu kiasi kama inavyoooonekana happo juu ili uweze kukata maumbo mbalimbali.Picha|King Arthur Baking.

Endelea kukoroga kisha uogeze ‘baking powder’ robo kijiko, vanila kijiko kimoja na  uchanganye vizuri. kama mchanganyiko mgumu weka maziwa au maji kiasi na uchanganye kwa dakika tano zaidi.

Baada ya hapo sasa ni wewe kukata maumbo unayotaka kama ni mduara, pembe tatu, kopa, nyota,au umbo lolote utakalo penda niwewe tu.

Ikiwa hauna Oven unawea kutumia jiko la mkaa, japo utahitajika kuwa makini zaidi iliusiunguze.Picha|Tasting table.

Jinsi ya kuoka 

Paka siagi katika sufuria au chombo utakachotumia kuoka, weka biskutii zako na uchome katika oven kwa  moto wa 120 kwa dakika 10 mpaka 15  na unaweza kuzitoa pale ukiona rangi imeanza kabadilika na kuwa brown.

Mpaka hapo biskuti zako zitakuwa tayari kuliwa.

© Copyright 2021 JikoPoint by Nukta Africa