Kuhusu sisi

Jiko Point ni jukwaa maalum na la kipekee la mtandaoni linalomilikiwa na kampuni ya Nukta Africa na kuwezeshwa na Shirika la Hivos na washirika wake kwa lengo la kuchochea matumizi ya nishati safi Tanzania. Ina vipengele vitatu ambavyo ni Jiko Class, Jiko News na Jiko Sokoni. 

Kwenye Jiko Class na Jiko News utapata habari za mapishi ya vyakula mbalimbali, madarasa ya mapishi na namna ya kutengeneza aina mbalimbali za nishati safi na vifaa vyake pamoja na matumizi mazuri ya nishati safi. Utasoma kozi kutoka kwa wakufunzi na wapishi mashuhuri hadi kupata vyeti kwa ama bure au gharama nafuu. 

Ndani ya Jiko Sokoni wafanyabiashara wanapata fursa ya kuuza vifaa na huduma za nishati safi mtandaoni kama majiko banifu, gesi ya kupikia na mkaa mbadala kuchochea matumizi ya nishati safi. Hii ni fursa adimu ya wanawake na wanaume wanaojikita kwenye biashara ya nishati safi na utunzaji mazingira kuwafikia wateja wengi zaidi na kwa urahisi. 

Kwa maulizo tutumie barua pepe [email protected] or Whatsapp +255 677 088 088. 

© Copyright 2021 JikoPoint by Nukta Africa