Jinsi ya kupika mchicha wa nazi na karanga

Na Lucy Samson
7 Jun 2024
Mboga hii inaweza kuliwa na wali, ugali chapati au ukala hivyo hivyo kama saladi kwa wale waliopo katika programu za kupunguza uzito.
article
  • Mboga hii itakupa ladha tamu na kukupa virutubisho muhimu vinavyoweza kujenga mwili wako.

Inawezekana umeshawahi kula mchicha lakini leo ngoja tujifunze kitu tofauti.

Ni mchanganyiko wa mchicha, nazi pamoja na karanga ambapo mbali na kukupa ladha tamu vitakuhahakikishia virutubisho muhimu vinavyoweza kujenga mwili wako.

Naam! Namaanisha vingi wa vitamini C vilivyopo kwenye mchicha, vitamin C na B vilivyopo kwenye Karanga pamoja na nazi ambavyo vyote vina faida nyingi mwilini.

Tuingie jikoni

Kama kawaida mapishi yetu huzingatia usafi hivyo anza kwa kuchambua mchicha kisha uoshe na uweke katika chombo kisafi.

Endelea na maandalizi yako kwa kukakata kata ikiwa unapendelea na ikiwa hupendi basi unaweza kuacha kama ulivyo ukahamia kuandaa nyanya, kitunguu maji, karannga za kusaga na nazi ambayo unaweza kuinunua dukani kuanzia Sh 1,000 ikiwa tayari kwa matumizi.

Baada ya hatua hizo basi sasa uko huru kuwasha jiko na kuinjika sufuria jikoni, ikipata moto weka mafuta kisha usubiri yachemke ndipo uweke vitunguu.

Ni vyema kuuosha vizui mchicha kabla ya kukata kata ili kuepuka kula mboga yenye michannga au vijidudu.Picha|Open Kitchen.

Kaanga vitunguu mpaka viwe na rangi ya kahawia kisha uongeze nyanya na uzipike mpaka ziive. Katika hatua hii unaweza pia kuweka viungo vya mchuzi na kitunguuu swaumu ikiwa ni kitu unachopenda.

Nyanya zikiiva weka mchicha, ufunike kwa dakika mbili mpaka tano unywee kiasi kisha unaweza kuweka karanga za kusaga kijiko kimoja (unaweza kuongeza kama mchicha ni mwingi) na ikichemka kidogo weka nazi nusu kikombe cha chai kisha funika kwa dakika nyingine tatu uive.

Malizia kwa kuweka chumvi, na pilipili kwa mbali ili ilete harufu kisha mboga yako itakuwa tayari kwa kula.

Mboga hii inaweza kuliwa na wali, ugali chapati au ukala hivyo hivyo kama saladi kwa wale waliopo katika programu za kupunguza uzito.

© Copyright 2021 JikoPoint by Nukta Africa