‘Icing sugar’ ni sukari laini ambayo hutumika kunogesha mapishi mbalimbali ikiwemo keki, mikate na baadhi ya vinywaji baridi.
Kwa wapenzi wa keki au wapishi ya kitafunwa hicho wanafahamu kuwa Icing sugar ni kiungo muhimu ambacho husaidia keki kuwa na muonekano mzuri ambao huvutia walaji.
Katika baadhi ya masoko nchini Tanzania bidhaa hiyo huuzwa kwa Sh5,000 hadi 10,000 kwa boksi lenye ujazo wa nusu kilo (500 kg) kutegemea na eneo ulilopo.
Ili kuepuka gharama hizo unaweza kuamua kutengeneza kiungo hicho nyumbani ili uweze kupamba keki na vitafunwa vyako kiurahisi.
Mahitaji utakayotumia ni sukari nyeupe, ‘cornstarch’ (sehemu ya unga wa mahindi) pamoja na blenda ya kusagia vitu vikavu.
Maandalizi
Anza kwa kuandaa sukari utakayoitumia, unaweza kununua kiasi chochote unachohitaji kulingana na mahitaji yako, ila hakikisha sukari yako ni kavu haina maji maji wala unyevu.
Baada ya kuiandaa, mimina kwenye blenda ya kusagia vitu vikavu, ongeza cornstarch vijiko viwili kwa kila nusu kilo ya sukari kisa usage kwa dakika tano hadi 10.
Rudia hatua hiyo mara nne hadi tano mpaka uhakikishe sukari imekuwa unga laini kisha uchekechekwa kutumia chujio lenye vitobo vidogo vidogo ilikupata ungalaini zaidi.
Ukihakikisha sukari yako imelainika kwa kiwango unahitaji Icing Sugar yako itakuwa tayari kwa kutumiwa.
Ili uweze kuitumia icing sugar kwa muda mrefu inashauriwa kuhifadhi sehemu kavu isiyo na unyevu katika chombo au mfuko usipitisha hewa.
Usikose kufuatilia makala ijayo ambapo tutajifunza jinsi ya kupika maandazi ya Icing sugar.