Maboga! ndiyo jina maarufu linalotumika kukitambulisha chakula hiki ambacho hutumiwa na wengi kama sehemu ya kifungua kinywa.
Wapo wanaotumia msosi huu kutengeneza rosti inayowekwa nazi, na viungo mbalimbali pia wapo wanaolichanganya na nyama lengo likiwa kuondoa ile dhana kwamba imsosi huo ni kwa ajili ya watu wa kijiji pekee.
Wakati waumini wa dini ya kiislamu wakibakisha miezi kadhaa kuingia katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, jikopoint tumekusogezea aina mpya ya mapishi ya maboga unayoweza kuandaa kwa urahisi nyumbani.
Ili kupika pishi hili utalazimika kunuua maboga ambayo masoko mengi huuza kuanzia Sh1,000 hadi 3,000 kutegemea na ukubwa.
Usisahau kuwa mbegu za maboga zinazobaki unaweza kuzitumia kama chanzo cha mapato kwa kuzikanga na kuziuza au ukazitumia kutengeneza unga wa lishe kwa ajili ya watoto.
Tuingie jikoni
Tuanze mapishi kwa kununua maboga kiasi ukioendacho kulingana na mahitaji yako, kisha osha maboga vizuri na uondoe maganda ya juu ambay mara nyingi huwa magumu.
Baada ya hapo kata maboga yako katika vipande vidogo vidogo kiurefu kisha weka kwenye bakuli lako safi.
Washa jiko, bandika maji jikoni weka chumvi kiasi kisha mimina maboga na uyaache yaive kiasi bila kulainika sana.
Hatua hiyo ikikamilka, yatoe jikoni na uyaache yapoe kwa dakika tano, kisha uendelee na hatua nyingine kwa kupasua mayai na kuyakoroga vizuri kisha kuyachanganya na maboga.
Ukihakikisha yamechanganyika vizuri bila kupondeka yatoe yaweke kwenye sahani na uyanyunyizie unga wa ngano na pilipili manga kiasi.
Lengo la kuweka unga wa ngano na pilipili manga ni kuongeza ladha na kulifanya likauke vizuri kabla ya kukaanga kwa sababu maboga huwa na maji mengi.
Endelea na mapishi kwa kuyangakaanga maboga ambayo tayari umeshayachanganya na mayai na unga wa ngano, hakikisha uamekaangika vizuri na uanze kuyaunga na viungo ambavyo tayari umeshaviandaa.
Anza kwa kukaanga kitunguu, kikiiva weka karoti na pilipili hoho na nyanya yako ya pakti au za kawaida na ufunike ziive vizuri.
Zikiiva weka mabogayaliyoakangwa na kukauka vizuri kisha koroga na uongeze viungo vingine vya mchuzi namaji kisha uache ichemke kwa dakika 10.
Muda huo ukipita angalia kama maji yamekauka na kutengeneza rojo nzito kiasi chako kisha itakuwa tayari kwa kuliwa.