Plastiki kwenye Microwave: Salama, si salama?

Na Tulinagwe Malopa
7 Feb 2022
Baadhi ya watu wamekuwa wakidai kuwa matumizi ya vyombo vya plastiki kupasha chakula kwenye microwave siyo salama kwa afya ya binadamu kwa sababu ni moja ya kisababishi cha saratani.
article
  • Wanasayansi wanasema plastiki haitengenezwi na kemikali za Dioxin bali Bisphenol- A na phthalates.
  • Wanasayansi wamesema kemikalihizo hazina madhara ya moja kwa moja. 
  • Madaktari washauri kutumia vyombo vya udongo kupasha chakula. 

Huenda ukawa mmoja ya watu wanaotumia mashine za kupashia chakula (Microwave) kwa ajili ya matumizi ya nyumbani au unapokuwa katika mazingira ya kazi. Matumizi haya yanategemea na chombo kinachotumika na mtu kulingana na mazingira aliyopo.

Baadhi ya watu wamekuwa wakidai kuwa matumizi ya vyombo vya plastiki kupasha chakula kwenye microwave siyo salama kwa afya ya binadamu kwa sababu ni moja ya kisababishi cha saratani.

Hata hivyo, Shule Kuu ya Udaktari ya Chuo Kikuu cha Havard cha nchini Marekani, katika moya ya andiko  kuhusu matumizi ya vyombo vya plastiki (Microwaving food in plastic: Dangerous or not?) linaeleza kuwa dhana hiyo kwa undani kuwa sio kila chombo chenye asili ya plastiki ni hakifai  kwa matumizi katika mashine hizo za kupashia chakula.

Andiko hilo limekanusha madai ya kwamba plastiki hutoa kemikali inayotokana na uchafu wa mazingira (Dioxin) na kuingia kwenye chakula wakati wa kupasha ambayo siyo nzuri kwa afya ya binadamu. 

Badala yake wamesema kemikali ya Dioxin haipo katika vyombo vya plastiki hivyo hakuna kemikali kama hiyo inayoingia kwenye chakula wakati wa upashaji kwenye mashine hizo.

Plastiki hukamilishwa kwa kemikali zinazozalishwa viwandani  (Bisphenol- A na phthalates) na mara nyingi hutumika katika uzalishaji wa chupa za maji, ambazo ndizo hukamilisha bidhaa ya plastiki sambamba na nyenzo zingine. 

Kwa namna moja au nyingine andiko hilo halijasema plastiki haina madhara kwa matumizi ya kupasha chakula badala yake matumizi yake yanatakiwa kuangaliwa kwa ukaribu na kuhakikisha chakula kinapashwa kwa moto usio mkali sana.

Bado matumizi ya plastiki yanaweza kuwa na athari kwa afya ya binadamu kwa sababu kemikali zinazokamilisha plastiki, zinaweza kuyeyuka na kuingia kwenye chakula wakati wa upashaji na kusababisha matatizo ya kiafya.

Kwa vyombo vya plastiki, hakikisha unachotumia kimewekewa nembo aya kutumika kwenye microwave. Picha| Shutterstock.

Hata hivyo, ametoa ushauri unaoweza kutumika katika kupasha chakula badala ya vyombo hivyo vilivyotengenezwa na plastiki.

“Binafsi naweza kushauri matumizi ya vyombo vya udongo kuliko plastiki kwa sababu madhara yaliyopo katika vyombo vya plastiki ni makubwa na mabaya kwa afya ya binadamu,” amesema Dk Sultan.

Madhara ya matumizi ya plastiki yanaweza yasionekane kwa haraka lakini ni kinga inayotakiwa kuzingatiwa katika hatua za awali kabla madhara hayajatokea baadaye.

Hata hivyo, baadhi ya wataalam wa afya wameiambia www.nukta.co.tz kuwa matumizi ya vyombo vya plastiki kupashia chakula kwenye microwave yana athari nyingi ambazo siyo rahisi kuzitambua. 

Daktari wa mafunzo ya mazoezi tiba katika Chuo cha Tiba na Sayansi Shirikishi Moshi (KCMC), Dk Joshua Sultan amesema matumizi ya plastiki kwa ujumla katika kupasha chakula siyo sahihi kwa afya kwa sababu ya kemikali zilizo ndani ya plastiki.

“Matumizi ya plastiki katika upashaji chakula siyo nzuri kwa sababu ya kemikali zilizotengenezwa ndani ya plastiki hiyo na madhara yake ni makubwa yanayoweza kusababisha saratani za aina mbalimbali”, amesema Sultan.

Kwa mujibu wa Dk Sultan amesema matumizi ya plastiki huweza kusababisha saratani za aina tofauti kama saratani ya koo ambayo ndio saratani inayosababishwa mara nyingi.

© Copyright 2021 JikoPoint by Nukta Africa