Juisi ya fenesi: faida na maandalizi yake

Na Mlelwa Kiwale
16 Aug 2024
Fenesi ni miongoni mwa matunda matamu yanayovutia wengi kuanzia kwenye ladha hadi rangi yake ya ndani. Tunda hilo lenye rangi ya kijani kwa nje na rangi nyeupe au njano iliyofifia kwa ndani, ambalo uliwaji wake ni wa ufanisi mkubwa linaweza pia kutumika kutengenezea juisi tamu itakayoburudisha familia au wageni watakokutembelea. Juisi hii pia inafaida nyingi […]
article
  • Uliwaji wake ni wa ufanisi mkubwa
  • Unaweza kunywa juisi yako kwa chakula chochote ukipendacho

Fenesi ni miongoni mwa matunda matamu yanayovutia wengi kuanzia kwenye ladha hadi rangi yake ya ndani.

Tunda hilo lenye rangi ya kijani kwa nje na rangi nyeupe au njano iliyofifia kwa ndani, ambalo uliwaji wake ni wa ufanisi mkubwa linaweza pia kutumika kutengenezea juisi tamu itakayoburudisha familia au wageni watakokutembelea.

Juisi hii pia inafaida nyingi ambazo huupa mwili virutubisho muhimu ikiwemo Vitamini na madini chuma jambo linalofanya kutumiwa na watu wa rika zote.

Bila kupoteza muda tuanze maandalizi ya juisi ya fenesi yanayoweza kuchukua wastani wa dakika tano hadi 15 kulingana na wingi wa juisi unayotengeneza.

Maandalizi 

Hatua ya kwanza utayaosha matunda na kuanza kuyaandaa vizuri huku ukitoa zile tunda zinazopatikana katika fenesi, kisha utachukua blenda yako na kuikagua kama ni safi kwa ajili ya matumizi.

Baada ya hapo utaweka fenesi, passion (karakara), parachichi, hiliki, sukari na maji kwa pamoja katika blenda na kuanza kuvisaga kwa muda wa dakika sita hadi viwe laini na kuchanganyika vizuri.

Tumia blenda kwa muda wa dakika sita, ukipumzisha kila baada ya dakika moja ili kuepusha blenda kupata moto sana na kuharibika.

Utaendelea na hatua hiyo hadi utakapomaliza mchanganyiko huo wa matunda na viungo vyako. 

Baada ya kumaliza kusaga utachuja hiyo juisi, kisha utahifadhi katika chombo kisafi na kama utapendelea utaweza weka katika friji (jokofu) lako ili iwe ya baridi au unaweza kunywa angali ipo hivyo hivyo.

Unaweza kunywa juisi yako kwa chakula chochote ukipendacho au hata pekee bila ya chochote.

© Copyright 2021 JikoPoint by Nukta Africa