Bei ya jumla ya maharage katika mikoa ya Mwanza na Lindi imepanda na kufikia Sh360,000, jambo linalonufaisha wafanyabiashara na wakulima wanaopeleka mazao kwenye mikoa hiyo.
Bei hiyo iliyorikodiwa kwenye mikoa hiyo ni ya jumla kwa kila gunia la kilo 100.
Takwimu za mazao makuu ya chakula zilizotolewa leo Octoba 5, 2022 na Wizara ya Viwanda na Biashara zinaonyesha kuwa bei inayotumika katika mikoa hiyo miwili ndiyo bei ya juu kuliko maeneo mengine nchini.
Pia bei wanayonunua wakazi wa mikoa hiyo ni mara mbili ya inayotumika mkoani Iringa.
Wakazi wa Iringa wananunua gunia la kilo 100 la maharage kwa Sh180,000.
Maharage ni miongoni mwa mazao makuu ya chakula nchini Tanzania.