Bei ya ngano bado kitendawili mkoani Lindi

Na Fatuma Hussein
11 Oct 2024
Kununua gunia la ngano la kilo 100 mkoani Lindi itakulazimu kulipa Sh400,000 ikiwa ndiyo bei ya juu zaidi kurekodiwa nchini Octoba 11,2024.
article
  • Yafikia Sh400,000 kwa gunia la kilo 100.

Kununua gunia la ngano la kilo 100 mkoani Lindi itakulazimu kulipa Sh400,000 ikiwa ndiyo bei ya juu zaidi kurekodiwa nchini Octoba 11,2024 ambayo ni sawa na bei iliyorekodiwa Septemba 2, mwaka huu.

Bei hiyo ni mara tano zaidi ya ile iliyotumika mkoani Rukwa ya Sh70,000 kwa gunia la kilo 100 la bidhaa hiyo muhimu katika kuandaa vitafunwa vinavyotumika katika maisha ya watu kila siku.

Wakati Lindi wakilia na ngano, wakazi wa Ruvuma na Iringa kwao ni vicheko baada ya gunia la kilo 100 la mahindi kuuzwa kwa bei ya chini ya Sh48,000 ambayo ni mara 20 zaidi ya bei iliyorekodiwa mkoani Dar es Salaam, Kilimanjaro na Pwani ikiwa ni ya juu zaidi.

© Copyright 2021 JikoPoint by Nukta Africa