Badala ya zawadi za kawaida kama nguo, manukato au maua, kwa nini usichague zawadi inayorahisisha maisha ya kila siku?
Pressure cooker (jiko la umeme lenye presha) ni zawadi ya kipekee inayochanganya upendo, vitendo na fikra za kisasa za kupika haraka, kuokoa nishati, na kulinda mazingira.
Ikiwa unatafuta zawadi ya maana kwa krismasi au mwaka mpya jikopoint tunakupa chaguo sahihi ambalo unaweza kuwafurahisha wapendwa wako msimu huu.
Kwa nini ‘pressure cooker’ ni zawadi kamili kwa familia?
Pressure cooker hurahisisha upishi kwa kupunguza muda wa kupika kwa kiasi kikubwa.
Familia zinaweza kuandaa chakula kwa haraka bila kukaa jikoni kwa muda mrefu, jambo litakalo wapa muda zaidi wa kupumzika na kufurahia sikukuu pamoja.

Ikilinganishwa na njia za jadi za kupika, pressure cooker hutumia nishati kidogo sana.
Hii inasaidia kupunguza matumizi ya kuni, mkaa au mafuta mengi, hivyo kupunguza gharama za kila siku za upishi.
Kwa familia nyingi, hii ni faida kubwa kiuchumi na katika mazingira yanayowazunguka.
Ni zawadi inayohamasisha matumizi ya nishati safi na maisha endelevu. Hatua ndogo kama hii ina mchango mkubwa katika kulinda mazingira kwa vizazi vijavyo.
Hii inaifanya pressure cooker kuwa chombo bora kwa familia zinazojali afya bora na lishe.
Sio hilo tu, inakoa muda katika upishi wa mapishi magumu, kama nyama, maharage, makongoro, supu, njugu, kunde, na hata mbaazi.
Kwa mfano ukihitaji ya pressure cooker la automatiki unalipata kwa Sh160,000 ndani ya msimu huu wa sikukuu huku ile ya kawaida (manual) ikipatikana kwa Sh150,000 ndani ya jikopoint na kwa wakazi wa Dar es Salaam usafiri ni bure.
Zawadi hii pia huongeza uelewa wa familia kuhusu umuhimu wa kuacha matumizi ya kuni na mkaa, jambo linaloboresha afya na mazingira ya nyumbani.
Kwa kifupi, pressure cooker si zawadi ya kawaida ni uwekezaji wa muda, afya, fedha na mazingira.
Hata hivyo, ukiachana na pressure cooker unaweza pia kutoa zawadi nyingine kama vile oveni, majiko ya umeme (induction cooker), blenda na hata jokofu.
Ikiwa unatafuta zawadi bora ya sikukuu, zawadi ya maana kwa familia, au vyombo vya jikoni vinavyookoa nishati basi usipoteze tena muda wako piga simu 0677088088 au tembelea katika tovuti ya www.jikosoni.co.tz.