Urojo ni mchanganyiko wa vyakula mbalimbali pamoja na uji uji wake katika bakuli moja.
Asili ya urojo ni kutoka nchini India lakini umejipatia umaurufu Tanzania pia. Leo nakupa maujanja ya kupika chakula hiki ambacho unaweza kutumia nyumbani na biashara.
Urojo wako ukiiva unaweza kuula na viazi mviringo vya kuchemsha, mayai ya kuchemsha, bagia, chachandu ya nazi, chipsi za muhogo, mishikaki, kachori, katlesi na pilipili.
Tuingie jikoni
Hatua ya kwanza weka unga kwenye bakuli kisha weka maji nusu lita pamoja na binzari. Baada ya hapo koroga hadi uhakikishe mabonge yote yameisha kisha mimina maji yaliyo baki kwenye sufuria na weka chumvi kiasi na uache yachemke kwa dakika 20.
Hatua inayofuata ni kumimina uji wenye binzari kwenye maji ya moto taratibu huku ukikoroga mpaka uchanganyike. Acha uchemke kidogo kwa dakika 5 kisha mimina ndimu yako na ukoroge kidogo na hapo unaweza onja chumvi na ndimu kama zipo sawa ndio utoe jikoni.
Kata viazi mviringo ulivyovichemsha vipande vidogo vidogo. Menya mayai kata vipande vinne, chukua bakuli na kijiko weka vipande vya viazi ulivyovikata.
Baada ya hapo malizia kuweka kachori, bagia, mishkaki, chipsi za muhogo na katlesi, kisha mimina urojo kiasi upendacho, weka chachandu ya nazi na pilipili.
Kufikia hapo urojo utakuwa tayari kwa ajili ya kutumiwa mezani.
Unataka tukufundishe pishi gani katika makala inayofuata? Dondosha maoni yako kupitia WhatsApp namba 0750 0881 888.
Angalizo: