Hapo vipi? Magimbi na nyama

Na Deycola Mutakyawa
2 Sept 2022
Magimbi husaidia katika kuimarisha afya ya ngozi, pamoja na kupunguza hatari kubwa ya kupata magonjwa kama vile kisukari.
article
  • Mlo huu unasaidia kuimarisha afya ya ngozi.
  • Ni rahisi kuandaa kama una mahitaji yote ikiwemo nyama na magimbi.

Magimbi ni miongoni mwa chakula kinachopendwa zaidi na watu hasa msimu wa Ramadhani. Hupatikana katika maeneo tofauti tofauti katika mikoa yote ya Tanzania.

Magimbi ni moja ya chakula cha asili kinachotokana na mmea unaoitwa mgimbi.

Imezoeleka kuwa chakula hiki huweza  kupikwa kwa kuchemshwa tu  lakini chakula hiki kinaweza kupikwa kwa namna nyingine tofauti  ya kuvutia na kuweza kuliwa.

Magimbi husaidia katika kuimarisha afya ya ngozi, pamoja na kupunguza hatari kubwa ya kupata magonjwa kama vile kisukari.

MAHITAJI

Nyama iliyochemshwa ½ kilo, magimbi  yaliyo menywa na kukatwa vipande ½ kilo, karoti, pilipili hoho, kitunguu, nyanya, kitunguu  swaumu, nazi,  chumvi, curry powder na pilipili manga.

MAANDAZI

  1. Weka vitunguu kwenye sufuria na vikaange na mafuta mpaka viwe rangi ya kahawia.
  2. Weka vitunguu swaumu, tangawizi mbichi, endelea kukaanga vitunguu visiungue.
  3. Weka Nyanya , subiri ziive, kisha weka karoti pamoja na hoho au pilipili mboga. 
  4. Weka curry powder, kisha weka chumvi kiasi, funika kwa dakika 2.
  5. Weka nyama iliyochujwa maji yote, kisha koroga vizuri ili nyama ichanganyike na viungo vingine.
  6. Kisha weka magimbi, na uweke nazi tui zito lililochanganyika na maji kisha funika mpaka kiive. Baada ya hatua zote magimbi ya nyama yatakuwa tayari kwa kuliwa.
© Copyright 2021 JikoPoint by Nukta Africa