Huenda kila mtu akawa na namna yake ya kupika kande za njugu mawe akiwa nyumbani. Wapo wanaopendelea kupika kwa jiko la gesi, kuni na wengine mkaa jambo.
Usikariri maisha! Ipo njia nyingine ya kupika kande kwa njia ya haraka na inayokoa muda wako wa mapishi. Ni kwa kutumia jiko lenye presha (Pressure Cooker) linalotumia umeme kidogo.
Kama bado hujafahamu ni pressure cooker lipi linalokufaa, JikoPoint inakushauri tumia la chapa ya WestPoint. Tazama video hii kujifunza zaidi.
Sasa tuendelee na pishi letu la leo la kande za njugu ndani ya pressure cooker. Unahitaji nini kukamilisha pishi hili? Mahitaji haya hapa:
Hatua kwa hatua; jinsi ya kupika kande za njugu mawe.
Hatua ya kwanza chambua mahindi na njugu mawe kwa makini ili kuondoa uchafu, mawe au vitu visivyofaa. Baada ya kuchambua, osha kwa maji safi ili kuondoa uchafu.
Hakikisha jiko lako la pressure cooker liko vizuri. Toa sufuria lilipo ndani na weka kande, njugu mawe, maji. Rudisha sufuri ndani ya jiko, kisha funga vizuri na mfuniko ili kutoruhusu presha kutoka nje. Washa jiko lako na weka muda unaotaka chakula chako kive. Hakikisha chakula na maji havizidi vipimo vilivyowekwa.
Chakula kikiva, kifaa chako kitajizima chenyewe baada ya muda kuisha, subiri kwa takriban dakika 10 hadi 15 ili presha iishe yenyewe na valvu ya kuelea irudi chini (Kama unatumia manual pressure cooker) ama waweza kuzungusha valvu ya presha kwenda kushoto ili kuondoa presha ikiwa una haraka.
Fungua mfuniko na ongeza karoti, hoho, vitunguu, mafuta ya kupikia na chumvi kiasi. Hakikisha viungo ulivyoweka vimechanganyika vizuri na kande zako. Funika mfuniko na washa tena jiko lako kwa kwa dakika 5 hadi 10.
Baada ya dakika 10, fungua mfuniko na ongeza tui la nazi na koroga taratibu kisha acha mchanganyiko uchemke kwa dakika 5 bila kufunika.
Mpaka kufikia hatua hiyo msosi wako utakuwa tayari kwa kuliwa hivyo unaweza kutoa jikoni na kufaidi na familia au wateja wako.
Kande za njugu zinafaa kuliwa zikiwa za moto kiasi. Unaweza kuongeza mchuzi wa nyama ukipenda lakini siyo lazima.
Unasubiri nini? Pressure Cooker ndio habari ya mjini kwa sasa. Okoa muda na gharama za nishati, pika kande kwenye pressure cooker.