Huenda umetamani kupika kuku wa kupaka kwa muda mrefu bila mafanikio huku woga na wasiwasi vikikusababisha ushindwe kujaribu.
Nikutoe wasiwasi, kuku wa kupaka ni moja ya mboga tamu na inavyopendwa sana na watu wengi hususani wanaotokea ukanda wa Afrika Mashariki.
Mapishi ya mboga hii yanaweza kufanyika katika nishati yoyote ila pressure cooker hupika kwa urahisi na uharaka zaidi.
Ikiwa hujawahi kupika kwa kutumia nishati hiyo makala hii ni kwa ajili yako ambapo tutapika mboga hii hatua kwa hatua hadi pale itakapoiva, cha kufanya ni kufuatana nasi hadi mwisho.
Mahitaji
Hatua kwa hatua namna ya kupika
Hatua ya kwanza katika pishi hili ni kuandaa kuku kwa kuanza kumuosha vizuri kisha kumkatakata vipande katika bakuli kubwa.
Baada ya hatua hiyo katika bakuli changanya vipande vya kuku na viungo vyote muhimu kabla ya kumpika ikiwemo chumvi, tangawizi, binzari, mchanganyiko wa giligilani na jira, pilipili ya unga na maji ya limao kisha muache kuku kwa angalau dakika 30, ili viungo vikolee vizuri
Baada ya dakika 30 katika sufuria la pressure cooker mimina mafuta kidogo kama vijiko viwili kisha kaanga vipande vya kuku vilivyokolea viungo (marinated) kwa muda wa dakika 10 au hadi pale vitakapo anza kubadilika rangi.
Ukimaliza kukaanga kuku na kupata rangi inayovutia mtoe jikoni kisha katika sufuria hiyo hiyo ongeza mafuta mengine kidogo, kaanga vitunguu maji vilivyokatwa hadi vianze kuwa na rangi ya dhahabu, kisha ongeza pilipili hoho ya kijani na paste (mchananyiko wa vitunguu saumu na tangawizi).
Ndani ya dakika mbili, katika mchanganyiko wako kwenye pressure cooker ongeza unga wa jira na binzari ya manjano, kisha koroga kwa sekunde 30 ili viungo visiungue kisha weka nyanya iliyokatwa na chumvi kwenye viungo na uache kwa dakika 7-10 na utie nyanya.
Hatua nyingine inayofuata baada ya kuweka nyanya zikaiva, mimina tui la nazi, koroga vizuri na uache mchuzi uchemke kwa dakika 5-7 nyingine bila kufunika pressure cooker.
Dakika 7 zikiisha na mchuzi ukiwa tayari umeiva vizuri, weka vipande vya kuku kisha acha vichemke kwa pamoja kwa dakika 3-5 ili kuku apate mchuuzi vizuri.
Mpaka hapo kuku wa kupaka atakuwa tayari kwa kuliwa unaweza kula kwa wali mweupe, chapati, au hata ugali.
Kama bado hujamiliki pressure cooker mpaka sasa, tembelea Jikopoint.co.tz ili uweze kujipatia pressure cooker ya westpoint kwa bei rahisi ya Sh170,000 kwa manual na Sh180,000 kwa digital.