Huenda bado unajiuliza Je, inawezekana kupika chakula cha kitamaduni kama machalari kwa kutumia pressure cooker?
Jibu ni ndiyo, teknolojia imerahisisha upikaji wa vyakula vya asili pasipo kupoteza ladha yake.
Zipo pressure cooker za aina mbalimbali. Leo tutamia chapa ya WestPoint kupika machalari (ndizi nyama) kwa haraka, usalama na bila usumbufu.
Kama bado hujaanza kutumia jiko hilo la umeme lenye presha, basi jikosokoni.co.tz wanayo dukani kwao, unaweza kujipatia moja kwa bei rahisi.
Basi tuendelee na pishi letu la machalari. Chakula hichi hutumiwa zaidi na watu wa kabila la Wachaga kutoka Kilimanjaro. Hata wewe unayependeza ndizi nyama, basi leo utaongeza ujuzi wa kupika kwa kutumia pressure cooker.
Jinsi ya kupika hatua kwa hatua
Hatua ya kwanza, anza kwa kuosha vizuri nyama kisha katakata vipande unavyopendelea.
Baada ya hapo, weka nyama ndani ya pressure cooker, ongeza chumvi na tangawizi iliyopondwa kisha mimina vikombe viwili vya maji. Bonyeza kitufe cha kupika nyama.
Kama unatumia pressure cooker ya kidijitali bonyeza kitufe kilichaandikwa ‘meat’ na kama unatumia ya manual zungusha kitufe mpaka sehemu inayoonesha dakika 15 za nyama.
Wakati nyama inaendelea kuiva, paka mikono yako mafuta kidogo ya kupikia kisha menya ndizi na viazi, kata vipande vya wastani na viweke kwenye bakuli lenye maji safi ili visibadilike rangi.
Hatua inayofuata andaa mahitaji mengine, safisha kitunguu maji, karoti na pilipili hoho, kisha vikate katika vipande vidogo kwa ajili ya kuongeza ladha kwenye chakula.
Baada ya dakika 15 za kupika nyama, iliruhusu presha itoke na fungua mfuniko na ongeza ndizi, viazi, viungo vyote pamoja na kijiko kimoja cha mafuta ya kupikia, koroga vizuri ili mchanganyiko ukae sawa, kisha funika tena na pika kwa dakika 10.
Baada ya dakika 10, toa tena pressure na fungua mfuniko, mimina tui la nazi kisha acha vichemke kwa dakika 5 bila kufunika.
Baada ya tui kuchemka, chakula kitakuwa tayari. Jumuika na wanafamilia mezani ili mfurahie chakula cha asili kilichopikwa kwa teknolojia ya kisasa.