Jinsi ya kupika maharage kwa muda mfupi

Na Wilson Malima
21 Jan 2022
Kwa kawaida, iwe ni maharage ya njano au mekundu (maharage kitenge kama wengi wanavyopenda kuyaita), kulingana na eneo mapishi yake yanahitaji saa moja hadi nne kuiva.
article
  • Watu wengi huogopa  kutumia gesi kupikia maharage.
  • Ni kwa sababu yanatumia muda mrefu kuiva.
  • Jifunze mbinu ya kuloweka maharage kabla ya kupika.

Maharage ni mboga ya wengi. Na hiyo ni kutokana na upatikanaji wake kuwa mwepesi na hata gharama yake kuwa rafiki kwa Watanzania.

Utamu wake na jinsi yanavyoshusha msosi kwa urahisi ni jambo lingine linalofanya mboga hii kushabikiwa na wengi. 

Kikwazo kikubwa ni muda wa kuiandaa mboga hii. Nikiwa mdogo nilimuona mama akitumia nusu siku kuchemsha maharage tu lakini leo, nitakufundisha mbinu za kupika maharage chap chap.

Kwa kawaida, iwe ni maharage ya njano au mekundu (maharage kitenge kama wengi wanavyopenda kuyaita), kulingana na eneo mapishi yake yanahitaji saa moja hadi nne kuiva.

Na hapo ndipo ugomvi wa maharage na matumizi ya gesi au umeme unapoanzia.

Nikutoe hofu, kuna njia nyingi za kupika maharage kwenye umeme na gesi na wala usihuzunike kutumia nishati hizo kuyaandaa.

kuloweka maharage husaidia kuyalainisha ili yaive haraka. Picha| Hum Nutrition

Loweka maharage kwenye maji

Chukua maharage kiasi ambacho umepanga kupika na kisha yaoshe. Weka maji kwenye chombo kulingana na kiasi cha maharage na ukubwa wa chombo kisha loweka maharage hayo. 

Funika mboga hiyo na uiweke sehemu salama na usubiri kwa saa sita.

Unaweza pia kuyaloweka kwenye maji ya moto ili kupunguza muda wa kusubiri.

Inashauriwa kuwa na chombo kinachohifadhi joto mfano chupa ya chai na hata “hot pot”.

Weka maji ya moto kwenye chombo hicho kisha maharage. Subiri kwa saa moja haddi tatu yatakuwa tayari.

Hadi hapo kumbuka tumechmsha maji tu.

Baada ya hapo, toa maharage yako tayari kwa kupika chap chap.

Wiki ijayo nitakufundisha mbinu za kuunga maharage kwa urahisi na sio kuyaandaa chuku chuku kama ulivyozowea. Natania tu, tutachangia maarifa.

Natumaini utaweka ratiba ya maharge katika mlo wako hakuna tena hofu ya kutumia nishati safi katika kuyapika.

© Copyright 2021 JikoPoint by Nukta Africa