Skonzi ni kitafunwa kinachopendwa na watu wengi hasa wakati wa asubuhi na mara nyingi huliwa kikiwa kimeambatana na chai, kahawa au maziwa.
Kutokana na upatikanaji wake kuwa rahisi hutumiwa pia katika shughuli mbalimbali ikiwemo ofisini..
Kuna aina nyingi za skonzi ambazo hutofautishwa kwa umbo, upishi na ladha zake. Zipo skonzi za zabibu, tende, chokoleti, vanila, nazi na nyama.
Katika maduka na migahawa ya kawaida kitafunwa hiki huuzwa kwa Sh500 hadi Sh1,000 na katika maeneo mengine huuzwa kwa Sh2,000 hadi Sh5,000 kutegemea na aina kitafunwa hicho.
Hivyo basi, ungana nami leo kupitia jikopoint.co.tz tujifunze jinsi ya kupika skonzi za maziwa tukitumia jiko la oveni.

Mahitaji
Jinsi ya kupika hatua kwa hatua
Anza kwa kuandaa unga wa ngano kwa kuuchuja na kuondoa makapi, na wadudu. Baada ya kuandaa unga chukua bakuli safi na kavu kisha weka ngano, sukari, hamira, baking powder robo kijiko pamoja na chumvi kisha uchanganye kwa dakika tano.
Hatua inayofuata chukua siagi yako kijiko kimoja na uichemshe ili iweze kuyeyuka kisha ichanganye kwenye unga wako. Siagi husaidia kulainisha, kuongeza ladha na harufu nzuri kwenye skonzi.
Ongeza maziwa pamoja na yai kisha uchanganye taratibu na kuanza kuukanda unga wako vizuri mpaka ulainike na kuwa donge lenye umbo la duara.
Funika donge lako na uweke mahali penye joto kwa dakika 10 hadi uumuke. Wakati ukisubri donge lako liumuke, chukua trei lako na upake siagi liwe tayari kwa ajili ya kuweka viduara vyako.
Angalia kama donge lako limeuumuka kisha kata maumbo ya viduara na uviweke kwenye trei, ziache mahali penye joto kwa dakika 15 mpaka ziumuke kwa mara ya pili.
Baada ya hapo, washa oveni na kisha nyunyizia ufuta juu ya skonzi zako.
Weka kwenye oveni kwa muda wa dakika 15 hivi kisha angalia kama zimebadilika rangi na kuwa za kahawia. Hapo skonzi zako zitakuwa zimeiva na zitakuwa tayari kuliwa.
Unataka kuendelea kupata dondoo za mapishi? Basi endelea kufuatilia tovuti ya mapishi na nishati safi na salama ya kupikia ya jikopoint.co.tz.