Jinsi ya kutengeneza maziwa mazito ‘condensed milk’

Na Fatuma Hussein
28 Oct 2024
Jiko Pointi imekusogezea namna rahisi ya kuandaa maziwa mazito ambapo mahitaji yake ni lita moja ya maziwa na nusu kilo ya sukari,
article
  • Mahitaji yake ni maziwa na sukari,
  • Unaweza kutumia sukari nyeupe au ya kawahia.

Yawezekana umeshakutana na mapishi mengi  ambayo miongoni mwa mahitaji yake ya muhimu ni maziwa mazito au condensed milk kama yanavyofahamika na baadhi ya wapishi.

Katika baadhi ya maduka maziwa mazito huuzwa kuanzia Sh 3500 kwa ujazo kopo dogo huku gharama ya ujazo wa kati zikianzia Sh10,000 kulingana na kampuni ya bidhaa hiyo.

Kutokana na kukosekana kwa maziwa hayo, wengine hushindwa kuandaa aina za mapishi zinazohitaji maziwa hayo  bila kujua kuwa unaweza kuyaandaa nyumbani kwa namna rahisi.

Jiko Pointi imekusogezea namna rahisi ya kuandaa maziwa mazito yatakayokuwezesha kuandaa aina mbalaimbali ya mapishi yanayohitaji maziwa hayo. Utakachohitaji ni lita moja ya maziwa na nusu kilo ya sukari,

Mkate wa mzinga wa nyuki ni miongoni mwa mapishi yanayohitaji maziwa mazito ambayo humwagiwa kwa juu kuongeza ladha na mvuto.Picha|Shuna;s kitchen/Youtube.

Namna ya kuandaa.

Hatua ya kwanza ni kuandaa maziwa kwa kuyachuja na kuhakikisha hayana uchafu wowote kisha endelea kwa kuwasha jiko na kubandika sufuria safi jikoni ikifuatiwa na mafuta pamoja na sukari.

Unaweza kutumia sukari nyeupe au kahawia kulingana na upatikanaji wake pamoja na eneo ulipo.

Baada ya hapo acha maziwa yachemke kwa moto wa wastani kisha ukoroge mara kwa mara ili mchanganyiko usishikane au kuganda katika sufuria.

Sukari ikishayeyuka, punguza moto wa jiko huku ukiendelea kuchanganya mchanganyiko huo mpaka uwe mzito dakika 20 hadi 30.

Baada ya kupata uzito unaotaka unaweza kuondoa jikoni kisha kuhifadhi kwenye chombo kisafi au kifungashio ambacho kitahifadhi vizuri bila kuharibika.

Mpaka kufikia hatua hiyo maziwa mazito yatakuwa tayari kwa matumizi. Unaweza kuyahifadhi kwenye jokofu na ukayatumia kwa siku saba hadi siku 10.

© Copyright 2021 JikoPoint by Nukta Africa