Mwanza. Nyama ya utumbo ni kipande cha nyama inayotoka katika tumbo la wanyama kama vile ng’ombe, nguruwe, kondoo au mbuzi.
Tamaduni nyingi kote ulimwenguni zimekuwa zikitumia utumbo kwa muda mrefu kama chanzo cha protini watu. Hata kwenye migahawa hupendelea kuomba supu ya utumbo na chapati kama kitafunio.
Pamoja na faida hizo leo tunataka kuangalia namna supu hii ya utumbo inavyoandaliwa.
Andaa utumbo wako wa mbuzi au ng’ombe kilo moja, kitunguu saumu kilichosagwa robo kijiko cha chai na tangawizi iliyosagwa nusu kijiko cha chai.
Tuingie jikoni
Osha utumbo vizuri kisha katakata katika vipande vidogo kulingana na saizi unayotaka. Weka utumbo kwenye sufuria, weka limao, chumvi, kitunguu swaumu, tangawizi koroga vichanganyike vizuri.
Viungo husaidia supu kuwa na harufu na ladha nzuri. Baada ya hapo bandika sufuria lako jikoni na uweke maji ya kutosha. Funika na uuache uive vizuri. Ikiwa tayari ipua na anza kula unaweza kutafunia kwa chapati au mandazi.