Mambo ya kuzingatia katika mapishi ya keki 

Na Fatuma Hussein
8 Jan 2024
Hata kama ndio unaanza safari ya kujifunza kupika keki kwa ajili ya matumizi binafsi au biashara, makala hii itakusadia kujifunza kwa haraka.
article
  • Ni pamoja na kuzingatia vipimo na kutokoroga keki kwa muda mrefu.
  • Hata kama ndio unaanza kujifunza mbinu hizi zitakufanya upike keki bora zaidi.

Baada ya kujifunza aina ya kwanza ya upishi wa keki ya vanilla leo tusogee mbele zaidi ambapo tutaangazia  mambo muhimu ya kuzingatia katika upishi wa keki.

Wakati tunaendelea kujifunza mbinu hizi, ni vyema kufahamu kuwa duniani  kuna aina nyingi  za keki na zote zina mahitaji na upishi tofauti.

Kufahamu aina ya keki unayotaka kupika kutakusaidia kujua mahitaji muhimu, muda utakaotumia kupika na mbinu za kutumia ili keki yako iwe tamu.

Basi bila kupoteza muda tujifunze mbinu hizi ambazo zinawafaa hata wale ambao ndio wanaanza safari ya kujifunza kupika keki kwa ajili ya matumizi binafsi au biashara.

Ili kuepuka kutoa keki vibaya unaweza kuiweka kwenye friji kwa dakika chache kabla ya matumizi.Picha |Spoonful.
  1. Usikoroge mchanganyiko wa keki muda mrefu

 Umeshawahi kuona keki imebonyea kati kati? basi leo ni kufahamishe kuwa kubonyea huko husababishwa na kukoroga keki kwa muda mrefu wakati ukiwa umeshachanganya mahitaji yako yote..

Mbali na kuboonyea, kukoroga keki kwa muda mrefu hupunguza nguvu ya ‘baking powder’ (kiungo muhimu katika upishi wa keki) na kusababisha kushindwa kuumuka inavyotakiwa.

Pia ni vyema kuangalia ikiwa ‘baking powder’ imekaa muda mrefu au imeisha muda wake wa matumizi (expire date) kabla ya matumizi  ili kupata matokeo bora katika upishi wa keki.

  1. Usifunue keki mara kwa mara

Kama wewe ni miongoni mwa wapishi ambao wanapenda kufunua msosi wanaoandaa mara kwa mara basi katiika pishi lhili la keki ni lazima ufunge mkanda.

Wakati unapika keki hautakiwi kufunuliwa mara kwa mara ili kuzuia keki yako kubonyea au kushindwa kuiva vizuri. Ukitaka kujua kamaimeiva basi utafunua kidogo mara moja na kupenyeza kijiti kikavu ambacho ndicho kitakupa majibu kama imeiva.

Ukishaitoa kake iache vile vile na chombo chake ipoe ndipo unaweza kuitoa katika chombo chake na kuikata, ukilazimisha kuitoa ikiwa yamoto itamomonyoka na kupondeka.

Mchanganyiko wa keki hautakiwi kuwa mzito sana au mwepesi sana.Picha|Times Food.
  1. Zingatia vipimo 

Miongoni mwa makosa ambayo wapishi wengi wa keki wanayafanya ni kukosea vipimo, jambo linalowafanyawashindwe kupata matokeo sahihi.

Mathalanbaking powder’ ambayo ukiiizdisha keki huweza huchambuka kupita kiasi na kupondeka pondeka na kupiteza mvuto.

Mabli na baking powder kuna kipimo cha sukari, mayai, siagi au mafuta na unga ambavyo hutakiwi kuzidisha wala kupunguza kupita kiasi.   

Je una mbinu nyingine unataka kushare nasi? tutumie kupitia WhatsApp kwa namba 0750 881 888.        

© Copyright 2021 JikoPoint by Nukta Africa