Namna ya kuandaa nyama ya kukaanga

Na Mariam John
27 May 2022
Ikate nyama vipande vidogo vidogo Ichanganye na viungo mbalimbali ikiwemo saumu na tangawizi. Ikaange kwenye jiko la gesi au umeme. Kila mmoja anaponunua nyama anatamani kupika pishi lake ambalo analipenda. Wapo wanaopenda mchemsho, rosti na hata wale wenye kuchoma. Wote hawa wanapata radha ya nyama kutokana na maandalizi yao wanayotaka. Jikoni leo napenda tuandae nyama […]
article
  • Ikate nyama vipande vidogo vidogo
  • Ichanganye na viungo mbalimbali ikiwemo saumu na tangawizi.
  • Ikaange kwenye jiko la gesi au umeme.

Kila mmoja anaponunua nyama anatamani kupika pishi lake ambalo analipenda.

Wapo wanaopenda mchemsho, rosti na hata wale wenye kuchoma. Wote hawa wanapata radha ya nyama kutokana na maandalizi yao wanayotaka.

Jikoni leo napenda tuandae nyama ya ng’ombe ya kukaanga, kitoweo kinachopendwa na watu wengi. 

Maandalizi

Baada ya kununua nyama yako, hatua ya kwanza ni kuikatakata kwa vipande vidogo vidogo, kisha mimina kitunguu saumu na tangawizi iliyosagwa. Hatua ya tatu mimina kiungo cha manjano kiasi kwenye nyama yako.

Kama ni mpenzi wa pilipili kavu unaweza kuweka pia sanjari na pilipili manga kiasi. Kamulia limao kiasi na kama una masala weka kiasi.  Unaweza ukamimina na mtindi kidogo kama kijiko kimoja cha chakula.

Baada ya kuweka viungo hivyo na kuichanganya vizuri na iache kwa muda wa saa moja au hifadhi kwenye friji kwa muda wa saa 12 hadi 24 kama hauitumiikwa siku hiyo na kama utaitumia kwa siku hiyo unaweza kuikaanga.

Kabla ya kukaanga usisahau kuweka chumvi.

Baada ya kuweka vikolombwezo hivyo hatua  inayofuata ni kupasha mafuta moto anza kukaanga nyama hadi ziive.

Nyama hii ya kukaanga unaweza kula kwa ugali, wali na hata ndizi.

© Copyright 2021 JikoPoint by Nukta Africa