Njia rahisi ya kupika ‘half keki’

Na Fatuma Hussein
18 Jul 2024
Watu wengi wanapendelea kupika ‘half keki’ kwa sababu ni pishi ambalo halitumii nguvu nyingi katika uandaaji wake. Pia ni rahisi kupika hata kwa mtu anayeanza kujifunza mapishi. ‘Half keki’ ni kitafunwa kinachotengezwa kwa ngano ambacho wengine hukifananisha na maandazi. Kumbuka tu chakula hiki ni fursa ya biashara na matumizi ya nyumbani kwa sababu bei yake […]
article
  • Hamira sio lazima kuweka kwenye half kake.
  • Poza mafuta yako kila baada ya mpiko mmoja.

Watu wengi wanapendelea kupika ‘half keki’ kwa sababu ni pishi ambalo halitumii nguvu nyingi katika uandaaji wake. Pia ni rahisi kupika hata kwa mtu anayeanza kujifunza mapishi.

‘Half keki’ ni kitafunwa kinachotengezwa kwa ngano ambacho wengine hukifananisha na maandazi.

Kumbuka tu chakula hiki ni fursa ya biashara na matumizi ya nyumbani kwa sababu bei yake ni kati ya  Sh500 hadi Sh1,000 katika migahawa mbalimbali. 

Hata hivyo, bei hutofautiana kutoka eneo mmoja kwenda eneo lingine. Faida itategemea na eneo unalofanyia biashara na mapenzi ya watu kwa chakula hicho ambacho hutumiwa zaidi asubuhi kwa chai au juisi.  

Tuingie jikoni

Hatua ya kwanza ni kuchanganya unga wa ngano na vitu vyote (kasoro mafuta ya kuchomea) kisha ukande. Hakikisha unakuwa mgumu ila usiwe kama unatengeneza biskuti. 

Baada ya hapo sukuma na ukate maumbo uyapendayo (hakikisha unakata vipande vinene kiasi na sio kama maandazi) 

Hatua inayofuata ni kuziweka sehemu yenye joto na uache ziumuke kwa dakika 20 hadi 30.

Zikiumuka zikaange katika moto mdogo ili ziive mpaka ndani, kisha ziipue na uweke katika chujio ili kuondoa mafuta.

Mpaka hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa na kinywaji chochote.

Vitu vya kuzingatia

  • Hakikisha unatumia vipimo sahihi bila kusahau ‘baking soda’ 
  • Sio lazima kuweka hamira kwenye ‘half keki’
  • Kanda unga wako uwe mgumu hata kidole kishindwe kupenya.
  • Weka half keki zako kwenye mafuta kabla hayajapata moto.
  • Poza mafuta yako kila baada ya mpiko mmoja, (unaweza kuepua ili yapoe au ukaongeza mafuta ya baridi)
© Copyright 2021 JikoPoint by Nukta Africa