Huenda umezoea kupika nyama kwa kutumia mkaa, kuni au jiko la gesi. Vipi ukibadilisha nishati ya kupikia na ukapikia jiko la umeme lenye presha kwa lugha ya kigeni Pressure Cooker.
Huenda ladha ya nyama yako ikawa tofauti. Upishi wa nyama kwa Pressure Cooker ni njia rahisi na ya haraka ya kupika chakula. Pia huokoa muda na hutumia kiasi kidogo cha umeme ukilinganisha na gesi au mkaa.
Kwa kutambua faida hizo, leo nakuongezea ujuzi wa kupika rosti ya nyama kwa kutumia Pressure Cooker chapa ya West Point ambayo huuzwa na kusambazwa na kampuni ya teknolojia ya Nukta Africa iliyopo jijini Dar es Salaam.
Presure Cooker ziko za aina mbili: manual (kawaida) na automatic (kidijitali). Kwa rosti yetu ya nyama tutatumia, pressure cooker ya kidijitali.
Unahitaji nini ili kukamilisha pishi hili? Mahitaji ni haya:
Hatua kwa hatua namna ya kupika
Hatua ya kwanza ni kuandaa mahitaji muhimu ya kupikia ikiwa ni pamoja na kuosha viungo na nyama kisha kukataka vipande vidogo vidogo.
Hatua inayofuata, chukua nyama ambayo tayari umeiandaa kisha weka kwenye sufuria maalumu, weka chumvi, tangawizi na ajna moto ili kuipa ladha.
Wakati unaweka viungo, hakikisha sufuria halishiki maji upande wa nje ili kuepusha uharibifu wa jiko lako la umeme lenye presha.
Ukimaliza hatua hiyo rudisha sufuria ndani ya pressure cooker na chomeka jiko kwenye soketi ya umeme kisha washa, taa nyekundu itawaka kuashiria jiko liko tayari kwa kupika. Weka muda wa kupika chakula.
Baada ya muda wa kupika kuisha, jiko hujizima na kuacha mboga katika hali ya joto.
Subiri kwa takriban dakika 10 hadi 15 ili presha iishe yenyewe na valvu ya kuelea irudi chini ama waweza kuzungusha valvu ya presha kwenda kushoto ili kuondoa presha ikiwa una haraka.
Presha yote ikiisha unaweza kuunga mboga yako kwa kutumia pressure cooker hiyo hiyo.
Mpaka hapo mboga yako itakuwa tayari kwa kuliwa na unaweza kula kwa ugali, wali ama chapati.