Samaki wa kukaangwa: Kitoweo cha watu wengi kanda ya ziwa

Na Mariam John
28 Jan 2022
Kukaanga samaki hakuhitaji mambo mengi. Mafuta ya kupikia, vitunguu swaum, tangawizi, chumvi na pilipili manga.
article
  • Unachohitaji ni samaki, mafuta, viungo na nishati ya kupikia.
  • kuivisha chakula hiki ni dakika 20 tu.
  • unaweza kula mboga hii kwa ugali, ndizi, chipsi au wali.

Upo nyumbani na unawaza aina gani ya mboga ungependa kutumia katika mlo wako wa usiku au chakula cha mchana? Jibu ni moja tu Samaki wa kukaanga.

Mboga hiyo, ni kati ya nyingi zinazoweza kutumiwa na mtu yeyote kutokana na ladha yake tamu na ukweli wa kwamba, haitumii muda mrefu katika kuandaa.

Samaki ina protini ambayo ni mhimu katika kujenga mwili

Kuandaa mboga hii, haihitaji uwe na akili ya kurusha roketi. Unahitaji viungo muhimu na ndani ya dakika kadhaa, mlo wako utakuwa mwezani.

Njoo tupike

Mahitaji ya msingi ambayo wengi hupenda kutumia kwenye kuandaa mboga hiyo ni; 

1: Samaki 

2: Kitunguu swaumu

3: Pilipili manga

4: Samaki (fish) masala

5: Limao au ndimu

6: Chumvi 

7: Mafuta ya kupikia 

8: Tangawizi

Kumchanja samaki kunasaidia mboga hiyo kuiva haraka zaidi. Picha| Bear Naked Food.

Kwa haraka, unahitaji dakika 20 tu kuivisha mboga yako.

Anza na kuwaandaa samaki wako. Ni kwa kuwaparua magamba, kutoa utumbo na kumchanja kwenue sehemu za nyama.

Baada ya hapo, ni muda wa kumuongezea ladha samaki kwa kumwekea viungo ulivyoandaa.

Tengeneza mchanganyiko wa kitunguu swaumu, tangawizi, pilipili manga, limau na chumvi kwenye bakuli.

Baada ya hapo, mpake samaki mchanganyiko huo na kisha mwache kwa nusu saa.

Hakikisha viungo vimeingia kila mahala usije kula samaki anachumvi sehemu moja.

Weka mafuta kwenye karai au kikaango na injika kwenye jiko la gesi au umeme. kama umenunua mashine ya kukaangia (deep fryer) pia nayo ni poa.

Mafuta yakipata moto weka Samaki wako na umwache kwa muda ili aive. mgeuze upande baada ya kuona anaiva upande mmoja na hadi samaki wote atakapokuwa rangi ya kahawia, mweke kwenye chombo cha kuchuujia mafuta.

Kama utakula samaki huyo na ugai, unaweza kukata kachumbari yako saaafi kisha urudi utuandikie maoni ya mlo wako ulioandaa.

© Copyright 2021 JikoPoint by Nukta Africa