Sh500 milioni kuhamasisha nishati safi ya kupikia vijijini

Na David Mselewa
1 Jun 2022
Zitasaidia kufanya kampeni kubwa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia. Pia Kufanyia tafiti ili kubaini nishati bora ya kupikia. Serikali ya Tanzania imesema katika mwaka ujao wa fedha 2022/23 itatumia Sh500 milioni kwa ajili ya utekelezaji wa mipango mkakati na miradi ya matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia hasa maeneo ya vijijini. […]
article
  • Zitasaidia kufanya kampeni kubwa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.
  • Pia Kufanyia tafiti ili kubaini nishati bora ya kupikia.

Serikali ya Tanzania imesema katika mwaka ujao wa fedha 2022/23 itatumia Sh500 milioni kwa ajili ya utekelezaji wa mipango mkakati na miradi ya matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia hasa maeneo ya vijijini.

Waziri wa Nishati January Makamba akiwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara ya Nishati ya mwaka wa fedha 2022/23 bungeni jijini Dodoma leo (Juni, 1, 2022) amesema karibu asilimia 89 ya kaya zote nchini zinatumia kuni na mkaa kama chanzo kikuu cha nishati ya kupikia hivyo kusababisha uharibifu wa mazingira pamoja changamoto za kiafya.

“Tumetenga Sh500 milioni ili kufanya kampeni kubwa ya kuhamasisha matumizi bora ya nishati ya kupikia pamoja na tafiti za kubaini nishati bora ya kupikia, mifumo sahihi na vivutio vya kusambaza nishati safi ya kupikia katika maeneo ya vijijini,” Waziri Makamba ameliambia Bunge.

Katika mwaka wa fedha ujao utakaoanza Julai, 1, 2022, wizara hiyo imeomba kiasi cha Sh2.9 trilioni ili kutekeleza majukumu yake na miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.

Aidha wizara hiyo imesema katika mwaka ujao wa fedha wizara itaongozwa na vipaombele takribani 12 ikiwemo kukamilisha mazungumzo ya mradi wa kusindika na kuchakata gesi  asilia (LNG) mkoani Lindi pamoja kutekeleza miradi ya kupeleka nishati vijijini.

© Copyright 2021 JikoPoint by Nukta Africa