Ipi bora? ‘Pressure cooker’ ya kidijitali au ‘manual’

Na Fatuma Hussein
1 Jul 2025
Unaponunua pressure cooker ya chapa ya WestPoint kutoka jikosokoni.co.tz, unakuwa umechagua kifaa halisi, chenye ubora wa hali ya juu na kinachodumu kwa muda mrefu.
article
  • Zote zinarahisisha na kuokoa muda wa kupika chakula.
  • Ufanisi wake hutofautiana kulingana na matumizi.
  • Bei, muundo na vifaa vyake pia havilingani.

Teknolojia ya mapishi inaendelea kuboreshwa ili kukidhi mahitaji ya watumiaji wake. Miongoni mwa teknolojia hizo ni jiko la umeme lenye presha (pressure cooker). Jiko hili hurahisisha mapishi jikoni kwa sababu linatumia kiasi kidogo cha umeme.

Kuna aina mbili za pressure cooker: za kidijitali na manuali na zote zinahitaji umeme ili kufanya kazi, lakini ubora na ufanisi wake hutofautiana kulingana na chapa ya kifaa.

Kwa mfano, unaponunua pressure cooker ya chapa ya WestPoint kutoka jikosokoni.co.tz, unakuwa umechagua kifaa halisi, chenye ubora wa hali ya juu na kinachodumu kwa muda mrefu.

Afisa Mawasiliano wa WestPoint nchini Tanzania, Sharon Mpondachuma amesema kuwa uwepo wa chapa hii sokoni kwa muda mrefu imejizolea sifa ya uimara na uaminifu miongoni mwa wateja.

“Ni imara sana, kwanza ‘bland’ (chapa) zetu ni ‘original’ ( halisi) ambazo hazina ‘cop’ (bandia) na ni watu ambao tupo sokoni muda mrefu uimara wake ni uhakika lakini pia ndio maana tunatoa ‘warrant’ ya mwaka mmoja mteja anaponunua,’’ amesema Mpondachuma.

Leo tunaangazia kwa undani tofauti iliyopo kati ya pressure cooker ya ‘manual’ na ‘digital’

Matumizi

Pressure cooker ya dijitali ni rahisi kutumia hata kwa watu wasio na uzoefu mkubwa jikoni. Ina vitufe maalum vilivyowekwa kwa ajili ya mapishi tofauti kama wali, nyama, maharagwe, supu na samaki. Unachotakiwa kufanya ni kuweka chakula, kisha kubonyeza kitufe kinacholingana na aina ya pishi lako.

Kwa pressure cooker za manual, mtumiaji anatakiwa kuzungusha kitufe maalum ili kuweka muda wa kupika. Haina vitufe vingi, jambo linaloifanya kuwa rahisi kwa baadhi ya watumiaji. Inahitaji umakinii wakati wa kupika ili kuepuka kuweka muda ambao hauendani na pishi lilokusudiwa.

Pressure cooker hii ambayo unaweza kuipata kwa Sh 170,000 kutoka JikoPoint, haina vitufe vingi, jambo linaloifanya kuwa rahisi kwa baadhi ya watumiaji. Picha/ Fatuma Hussein JikoPoint.

Bei

Pressure cooker ya dijitali, chapa kama WestPoint, huwa na bei ya juu. Kwa mfano, kupitia tovuti ya jikosokoni.co.tz, unaweza kuipata kwa Sh180,000, ikilinganishwa na chapa nyingine zinazouzwa kwa bei ya juu zaidi. Hata hivyo, katika maeneo ya vijijini, upatikanaji wake unaweza kuwa changamoto.

Kwa upande wa manual, bei yake huanzia Sh160,000 hadi Sh170,000 kwa chapa ya WestPoint. Hata hivyo, wazalishaji wa chapa nyingine hawazalishi kwa wingi aina hii ya jiko la umeme lenye presha, hivyo upatikanaji wake unaweza kuwa mdogo.

Kwa mfano, kupitia tovuti ya jikosokoni.co.tz, unaweza kuipata kwa Sh180,000. Picha Goodluck Gustavo.

Idadi ya vitufe

Aina hii huwa na jumla ya vitufe 15 kwa chapa ya WestPoint, ambapo 11 ni vya mapishi tofauti, na vingine vina kazi maalum kama kuongeza muda, kuchelewesha muda wa kuanza kupika, au kupasha chakula moto.

Kwa ile ya manual Ina kitufe kimoja tu, ambacho huzungushwa ili kuchagua aina ya mlo unaotaka kupika. Ingawa ni rahisi kutumia, inahitaji mtumiaji kukadiria kwa makini muda unaofaa kwa kila chakula.

Uamuzi wa kuchagua kati ya pressure cooker ya dijitali au ya manual hutegemea mtindo wa maisha yako, bajeti yako, na urahisi wa matumizi. Kufahamu zaidi kuhusu majiko haya ya umeme yenye presha tembelea jikopoint.co.tz au piga simu kwa namba 0677 088 088.

© Copyright 2021 JikoPoint by Nukta Africa