Jinsi ya kuhifadhi pressure cooker idumu muda mrefu

Na Fatuma Hussein
5 Jun 2025
Baada ya kupika chakula, iache pressure cooker ipoe kwa kufungua valvu na mfuniko ili kutoa joto. Baada ya hapo, hifadhi sehemu salama.  
article
  • Ni pamoja na kuzingatia usafi ili kuepuka kupata matatizo ya kiufundi.
  • Hifadhi sehemu salama isiyo na unyevunyevu au ukungu  


Huenda wewe ni mtumiaji wa jiko la umeme lenye presha (pressure cooker) lakini hauna ujuzi wa njia sahihi za kutunza kifaa hiki.

Matumizi sahihi na utunzaji wa pressure cooker husaidia ifanye kazi kwa ufanisi na kudumu kwa muda mrefu.

Ikiwa Pressure cooker haitatunzwa na kuhifadhiwa vizuri, inaweza kupata matatizo ya kiufundi, kuharibika haraka au hata kusababisha ajali zisizotarajiwa.

Hivyo basi, leo ndani ya JikoPoint.co.tz tunakupa maujanja ya mambo ya kufanya baada ya kutumia pressure cooker ili idumu muda mrefu na ufanisi wake uwe wa kiwango kinachotakiwa. 

Hakikisha ni safi, kavu na iache ipoe baada ya kutumia

Baada ya kupika chakula, iache pressure cooker ipoe kwa kufungua valvu na mfuniko ili kutoa joto. Baada ya hapo, hifadhi sehemu salama.  

Pressure cooker inapaswa kuwa safi ili kuzuia mkusanyiko wa uchafu unaoweza kuleta harufu mbaya au kuvutia wadudu.

Safisha kwa umakini baada ya matumizi usafi huongeza uimara. Picha/ Goodluck Gustaph/ JikoPoint.

Ukavu wa Pressure cooker ni muhimu ili kuepuka kutu sehemu zake za chuma, kwani unyevunyevu unaweza pia kusababisha hitilafu za umeme ikiwa utahifadhiwa kabla ya kukauka. 

Onya vizuri mfuniko na sufuria. Pia safisha jiko kwa kitambaa kikavu na hifadhi sehemu salama.

Toa plagi ya waya wa umeme kutoka kwenye soketi iliyo nyuma ya pressure cooker

Kabla ya kuihifadhi Pressure cooker, ni muhimu kuiondoa kutoka kwenye chanzo cha umeme. Hii husaidia kuzuia shoti au uharibifu wa kifaa endapo kutakuwa na mabadiliko ya umeme.

Fungua mfuniko uweke pembeni ruhusu hewa iingie, epuka ukungu na harufu. Picha/ Goodluck Gustaph/ JikoPoint.

Kuondoa plagi husaidia kulinda waya wa umeme dhidi ya kukunjika au kuharibika unapokuwa umehifadhi kifaa. Hii pia hurahisisha kupanga kifaa vizuri kwenye eneo la hifadhi bila hitilafu.

Hifadhi sufuria ndani ya boksi au kwenye pressure cooker

Ukiosha sufuria ya kupikia ipukute kwa kitambaa kikavu kisha weka sehemu salama ikiwemo ndani ya pressure cooker.

Kuweka sufuria ndani ya koti lake kunapunguza uwezekano wa kupoteza vipande au kuvunjika wakati wa kuhifadhi.

 Ni njia salama ya kuhakikisha kifaa kinabaki kamili na tayari kwa matumizi ya baadaye.

Fungua mfuniko uweke pembeni ili kuruhusu pressure cooker kupata hewa.

Usifunge kabisa mfuniko wa juu wa pressure cooker baada ya matumizi. Badala yake weka pembeni kuruhusu hewa kuingia na kuzunguka ndani. 

Toa plagi kutoka soketini linda kifaa chako dhidi ya shoti ya umeme.Picha/ Goodluck Gustaph/ JikoPoint.

Inashauriwa kufungua au kulegeza valvu ya kifuniko cha pressure cooker pembeni baada ya kutumia ili kuruhusu hewa kuingia ndani. Pia unyevunyevu utaondoka na kupunguza harufu mbaya au ukungu.

Kufanya hivi kunasaidia pressure cooker yako ibaki katika hali nzuri kwa muda mrefu.

Weka pressure cooker mahali pasafi, pakavu, na pasipofikika na watoto

Mahali pa kuhifadhi panapaswa kuwa salama na pasipo na unyevunyevu, kwani mazingira yasiyo rafiki huweza kuharibu kifaa chako. 

Hifadhi kwenye boksi au ndani ya kifaa epuka kupoteza au kuvunjika. Picha/ Goodluck Gustaph/ JikoPoint.

Epuka maeneo ya wazi kama jikoni yenye mvuke mwingi au sakafu yenye unyevunyevu. Weka mbali na watoto ili wasiharibu. Uhifadhi salama huongeza maisha ya pressure cooker na kuzuia ajali zisizotarajiwa.

Usiweke kitu chochote juu ya pressure cooker

Usiweke kitu chochote juu ya pressure cooker linda kifuniko kisiharibike.Picha/ Goodluck Gustaph/ JikoPoint.

Kuweka vitu juu ya Pressure cooker kunaweza kusababisha kifaa kuharibika kwa kushinikizwa au kuvunjika.

Hali hii huenda ikaathiri mfuniko wa kifaa chako na kusababisha hasara za kufanya marekebisho au kununua kifaa kingine kifuniko.  Kama unasoma makala hii na bado hujamiliki pressure cooker, basi unaweza kujipatia kutoka jikopoint.co.tz au wasiliana nasi kupitia 0677088088.

© Copyright 2021 JikoPoint by Nukta Africa