Kama unataka njia rahisi na ya haraka ya kupika chakula, basi jiko la umeme lenye presha (Pressure Cooker) ndio suluhisho.
Hata hivyo, matumizi yasiyo sahihi ya kifaa hiki yanaweza kuhatarisha usalama wa mtumiaji na familia nzima. Ili kuhakikisha unatumia pressure cooker kwa njia salama na ya ufanisi, ni muhimu kufuata mwongozo wa matumizi na kuchukua tahadhari.
Haya ndio mambo muhimu ya kuchukua tahadhari wakati wa unatumia pressure cooker jikoni:
Usiwaruhusu watoto au watu wenye mahitaji maalum kuitumia bila uangalizi
Watoto walio chini ya miaka nane (8) na watu wenye mahitaji maalum ya kimwili au kiakili hawapaswi kutumia pressure cooker bila msaada au uangalizi wa karibu.
Kifaa hiki kinahusisha presha na umeme ambavyo vyote ni hatari kwa watumiaji wasio na uwezo wa kuelewa au kudhibiti mazingira ya matumizi.
Kwa usalama wa familia, ni muhimu kuweka pressure cooker mbali na watoto na kuhakikisha hakuna anayetumia bila maelekezo. Uangalizi wa mtu mzima ni wa lazima ili kuepuka milipuko inayoweza kusababisha madhara kwa mtumiaji..
Usafi ufanywe na mtu mzima mwenye uelewa
Usafi wa pressure cooker ni muhimu kwa kudumisha uimara wake na kuhakikisha hakuna mabaki ya chakula au unyevu vinavyoweza kusababisha kuharibika kwa kifaa.
Kazi hii haifai kufanywa na mtoto kwa sababu kuna maeneo ya kifaa yanayohusiana moja kwa moja na umeme. Mtu mzima mwenye uelewa wa namna ya kusafisha vifaa vya umeme ndiye anayepaswa kufanya usafi huu.
Kwa mfano, kusafisha bila kutenganisha sehemu zinazohitaji maji na zile za umeme kunaweza kusababisha kifaa kuharibika au hata mshtuko wa umeme wakati wa matumizi yajayo.
Usitumie kifaa kama waya umeharibika
Kabla ya kuwasha pressure cooker, hakikisha kuwa waya wake wa umeme haujaathirika kwa namna yoyote kama vile kukatika, kuchomwa au kuchubuka.
Waya wenye hitilafu unaweza kuwa chanzo cha moto au mshtuko wa umeme na kuleta madhara kwa mtumiaji.
Ni muhimu kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa waya na plagi za kifaa chako. Ikiwa kuna dalili zozote za uharibifu, ni bora kukiacha kifaa hicho na kupeleka kwa fundi mwenye utaalam au kuwasiliana na wauzaji kwa usaidizi zaidi.
Usioshe jiko la presha kwa maji
Pressure cooker hasa jiko lake halipaswi kuoshwa na maji. Ukifanya hivyo utaharibu mfumo wa umeme na kuiua kabisa.
Badala yake, tumia kitambaa safi au brashi laini kusafisha sehemu zinazoweza kufikiwa kwa urahisi bila kuhatarisha umeme.
Usiiwashe ikiwa haina chakula ndani
Unashauriwa usiwashe pressure cooker ikiwa haina chakula wala maji ndani ya sufuria. Kuwasha kifaa hiki bila kitu ndani kunaweza kuharibu sufuria kwa kuungua au kulika haraka, na hata kusababisha moto au mlipuko.
Hakikisha kila mara unapowasha jiko lako, unaweka kiasi kinachofaa cha chakula au maji ili kusaidia kupunguza matatizo yanayoepukika.
Hatua hizi ni msingi wa matumizi sahihi na salama ya jiko lako na huongeza muda wake wa matumizi.
Kwa kuzingatia mambo haya,kifaa chako kitaendelea kuwa salama wakati wote. Unapenda kujifunza au kumiliki pressure cooker ya hadhi yako, basi utaipata jikopoint.co.tz . Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa namba 0677 088 088..