Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda amesema kuwa mkoa huo umejioanga vyema kusherehekea siku ya wanawake dunaini kwa kutoa huduma mbalimbali ikiwemo za afya na sheria zitakazoambatana na uchomaji wa nyama kwa kutumia gesi.
Makonda ameyasema hayo wakati akizungumza katika mkutano wa tano wa Serikali mtandao e-Ga leo Februari 11, 2025 ambapo amesema kuwa lengo la kutumia gesi kuchoma nyama ni kuendeleza jitihada za kuhamasisha matumizi ya nishati safi nchini.
“Tumewaomba Waziri wetu wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu kuhakikisha tunatumia gesi safi ili wananchi waweze kuona tofauti kati ya nyama inayochomwa kwa nishati safi na ile inayochomwa kwa nishati isiyo rafiki kwa mazingira,” amesema Makonda.
Kwa mujibu wa kiongozi huyo, mpaka sasa wameshapokea ng’ombe 100 na tunatarajia kuwa na ng’ombe 500 pamoja na takriban nyama pori 100 ambao watachomwa na kuwa sehemu ya maadhimisho hayo.
Hii si mara ya kwanza kwa mkoa wa Arusha kuadhimisha hafla mbalimbali kwa kuchoma nyama, itakumbukwa mwishoni mwa mwaka 2024 Makonda aliytangaza sherehe za mwisho wa mwaka na kuupokea mwaka moya 2025 ambazo pia zilinogeshwa na nyama choma.
Tofauti ya maadhisho ya siku ya wanawake duniani yanayofanyika kitaifa jijini Arusha na maandimisho mengine yaliyowahi kufanyika ni matumizi ya nishati safi ya kupikia ambapo itaokoa muda kwa wapishi wanaotumia muda mwingi jikoni huku ikilinda afya zao.
Mbaliu na nyama choma, Makonda amesema maadhimisho hayo yatatnguliwa na shughuli mbalimbali ikiwemo upimaji wa afya bure kwa wananwake wajawazito pamoja na utolewaji wa msaada wa kisheria kwa watakaohitaji.
“Katika kipindi hiki cha siku saba, huduma maalum zitahusisha vipimo vya kitaalamu kwa wanawake wajawazito. Mtambo bora wa kisasa ulionunuliwa kwa juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan utatumika kugundua changamoto za moyo kwa watoto wakiwa tumboni…
…Wanawake wote wajawazito watafanyiwa vipimo, na wale watakaobainika kuwa na changamoto wataanza matibabu mara moja ili kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua,” amesema Makonda.