Oveni ni kifaa kinachotumia nishati kuchoma, kupika na kuoka baadhi ya vyakula ikiwemo keki.
Kifaa hiki hutumia nishati mbalimbali ikiwemo umeme, gesi, umeme jua na nyinginezo ambazo hutoa joto linalowezesha vyakula kuiva.
Umuhimu wa kifaa hiki katika kurahishsa shughuli za nyumbani umekifanya kuwa maarufu huku baadhi ya watengenezaji wakikiunganisha pamoja na majiko ya kawaida ya kupikia.
Licha ya umuhimu wake, kikitumiwa kwa muda mrefu huchafuka na kuwapa watumiaji wakati mgumu kuosha, baadhi wakihofia kuharibu mifumo ya umeme iliyopo au kupasua kioo kinachotumika kufunikia.
Jiko point imekuandalia hatua tatu muhimu zitakazokuwezesha kusafisha oveni yako bila ‘stress’ huku ikuweka mbali na harufu inayoweza kusababishwa na uchafu wa kifaa hicho.
Hatua hii ya kwanza inahusisha maandalizi ya vifaa vya usafi vya kawaida ambavyo vyote vinapatikana kwa urahisi nyumbani au madukani.
Vifaa hivyo ni kwa mujibu wa tovuti ya Hoovers ni ‘baking soda’, siki (vinegar), sabuni ya vyombo, glavu za mpira za kuvaa mikononi kama utahitaji. osheo na kitambaa cha kukaushia.
Baada ya kukusanya vifaa vyote ya usafi anza kutoa raki za kuokea ( oven racks) na uziloweke katika maji yenye sabuni pembeni, uzioshe na zikikauka uziweke pembemni kwa ajili ya matumizi baadae.
Endelea na usafi kwa kuondoa uchafu na mabaki ya vyakula ndani ya oveni kwa kutumia mkono au dodoki la kuoshea kisha utengeneze mchanganyiko wa siki pamoja na baking soda na upake ndani ya oveni na uache kwa muda wa masaa 12 ili uchafu ulioganda uyeyuke.
“Baada ya hapo, futa mabaki kwa kutumia kitambaa cha microfibre chenye unyevu. Pulizia siki nyeupe juu ya mabaki yaliyosalia na futa kwa kitambaa kingine safi kwa kumalizia usafi,” imsesema tovuti ya Hoovers.
Unaweza kumalizia usafi huo ndani ya oveni kwa kupasha moto Oveni kwa sentigredi 90 mpaka 120 kwa dakika 15 ili kuondoa kabisa uchafu na kuua kemikali za usafi zilizobakia.
Unaweza kurudia kufuta tena ili kujihakikishia kuwa ipo safi.
Kwa wapishi wanafahamu kuwa sehemu ngumu kuliko zote kusafisha ni kioo kinachotumika kama mlango wakati wa kupika pamoja na vitufe vya kuwashia.
Tovuti ya Realsimple inabainisha kuwa njia rahisi ya kuondoa uchafu uliokwama katikati ya vioo vya oveni ni kuifungua kwa ungalifu ukitegemeza vioo katika miguu yako.
“Hatua ya kwanza, fungua mlango wa oveni na uwekee juu ya mguu wako ili kuupatia msaada. Kisha, toa viskrubu kwenye sehemu ya juu ya mlango. (Kwa kuweka mlango juu ya mguu wako, utaepuka kuanguka na kuvunjika.) Baada ya kutoa viskrubu, utaweza kufikia sehemu za kati za mlango wa oveni,” imesema tovuti ya Real simple.
Baada ya kufungua unaweza kuviosha kwa sabuni na dodoki au kupakaza mchanganyiko wa siki na baking soda juu ya kioo na kuufuta baada ya 20.
Ukimaliza futa tena kwa kutumia kitambaa safi kisha urudishie srubu za vioo kama zilivyokuwa awali na kioo chako kitakuwa safi.
Usisahau pia kusafisha vitufe vya oveni ambavyo mara nyingi hubeba uchafu wakati wa kuwasha au kuzima.
Kwa kufata hatua hizo oveni yako itakuwa safi ikikuruhusu kuoka vyakula vingi zaidi kadri upendavyo.