Vileja vya tambi. Ndio! Ni aina ya chakula kinachopendwa na watu wengi kwa sababu kina aina mbalimbali ya mapishi.
Kuna vileja vya aina mbalimbali vikiwemo vya nazi, ngano na hata tambi.
Leo nitakufundisha kwa undani unavyoweza kupika vileja vya tambi na mambo ya kuzingatia ili kupata matokeo mazuri katika pishi lako.
Vileja hujulikana kama kashata lakini zinategemea umetumia bidhaa gani ya chakula kutengeneza.
Tuingie jikoni
Hatua ya kwanza ni wewe kuweka karai kwenye moto kiasi kisha weka siagi yako. Baada ya hapo weka tambi uzikaange na uziachie mpaka ziwe rangi ya dhahabu unaweza kutumia dakika 5 mpaka dakika 7.
Ongeza rozi na zabibu huku unakoroga kisha weka maziwa ukiendelea kukoroga. Ongeza arki ili kuongeza ladha.
Hatua inayofuata ni kuepua karai, tumia kijiko kuchotea na weka kashata zako kwenye kikombe cha kahawa nusu usikijaze kisha kipindue kwenye sahani utoe kileja.
Rudia hatua hiyo mpaka umalize vyote na ukimaliza vileja vitakuwa tayari kwa kuliwa.
Unasubiri nini? Leo andaa vileja vya tambi ili kuwafurahisha wapendwa wako nyumbani.