Jinsi ya kuandaa juisi, chai ya mchaichai

Na Lucy Samson
1 Jun 2022
Kinywaji hicho ni cha asili. Hutumika kutibu magonjwa ikiwemo kukata kitambi. Mchaichai kama ambavyo lilivyo jina lake, ni kiungo maarufu sana kinachotumiwa kwenye mapishi ya chai. Huifanya chai iwe na harufu nzuri na ladha ya kuvutia. Mbali na umaarufu wake kiungo hiki kinaweza kukupa muonekano wa ndoto zako. Kikitumiwa vizuri huweza kuondoa kitambi kabisa na […]
article
  • Kinywaji hicho ni cha asili.
  • Hutumika kutibu magonjwa ikiwemo kukata kitambi.

Mchaichai kama ambavyo lilivyo jina lake, ni kiungo maarufu sana kinachotumiwa kwenye mapishi ya chai. Huifanya chai iwe na harufu nzuri na ladha ya kuvutia.

Mbali na umaarufu wake kiungo hiki kinaweza kukupa muonekano wa ndoto zako. Kikitumiwa vizuri huweza kuondoa kitambi kabisa na kukuacha ukiwa na muonekano wa kuvutia. 

Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali zilizofanyika, mchaichai una faida nyingi mwilini kama kutibu magonjwa ya kichwa, kulinda figo na mashambulizi ya bakteria.

Hutibu mfumo wa mmengenyo, maumivu yatokanayo na hedhi, kwa mujibu wa jarida la afya la health line.

Mtaalamu wa afya na lishe, Matilda kambangwa anasema kinywaji hiki kinafaa zaidi kutumiwa wakati tumbo likiwa tupu (on empty stomach) mara nyingi ni asubuhi kabla hujala chochote.

Najua unajiuliza maandalizi ya kinywaji hiki. Ili uweze kutatua changamoto ya kitambi inayowasumbua wengi, katika makala haya nimekuandalia aina mbili za kutengeneza kiungo hiki,mchaichai kama juisi na mchai chai kama chai.

Aina zote mbili za uandaaji wa kinywaji hiki utakuwezesha kupata matokeo unayoyataka iwe ni kupunguza kitambi au kutibu changamoto yoyote ya afya.

Mchaichai kama chai

Aina ya kwanza ya kuandaa kinywaji hiki ni ile iliyozoeleka ya kuchemsha mchaichai na kuutumia kama chai. Hapa tutakuongezea mahitaji kadhaa na kuifanya iwe na virutubisho zaidi.

MAANDALIZI

Osha mchaichai na ukate vipande vya wastani vitakavyoweza kuingia kwenye sufuria au chombo chako utakachotumia kushemshia maji.

Andaa sufuria ya kuchemshia weka maji vikombe viwili,weka mchai chai, tangawizi na mdalasini kisha washa jiko na uache jikoni mpaka ichemke.

Ikisha chemka chuja weka sukari ongeza na vijiko viwili vya maji ya ndimu, hapo kinywaji chako kipo tayari.

unaweza kutumia kinywaji hiki kama kifungua kinywa (breakfast). Kwa kutatua shida ya kitambi hakikisha unakunywa dakika 40 au saa 1 kabla ya kula mlo mwingine wa asubuhi.

Mchaichai kama juisi

Namna ya pili ya kuandaa kinywaji hiki ni ile ya kusaga majani ya mchaichai  kwenye blenda, mahitaji ni yale yale kama ya mwanzo.

Juisi ya Mchaichai na Ndimu.Picha|Vanita’s corner.

MAANDALIZI

Osha majani ya mchaichai na uyakate vipande vidogo vidogo vitakavyo enea kwenye blenda.

Weka mchaichai kwenye blenda na maji vikombe 3 kisha saga mpaka upate mchaganyiko mzito kiasi.

Ukimaliza kusaga ongeza sukari,mdalasini, maji ya ndimu, tangawizi  na maji vikombe 3 kisha usage tena.

Baada ya hapo chuja na weka kwenye glas uongeze na vipande vya barafu mchaichai wako uko tayari kwa kunywa.

kinywaji hiki kinaweza kutumiwa wakati wowote, unaweza kuhifadhi kwenye jokofu kwa matumizi ya baadae

Kinywaji hiki kikitumika vizuri kinasaidia sana kutatua changamoto ya kitambi.

© Copyright 2021 JikoPoint by Nukta Africa