Huenda unafahamu kutengeneza juisi nyingi lakini juisi ya peasi ni nadra sana kuikuta sehemu nyingi wanaouza vinywaji.
Kwa mujibu wa tovuti ya Healthline peasi ni tunda lenye faida nyingi ikiwemo kuukinga mwili kutokana na magonjwa sugu, kudhibiti kiwango cha sukari pamoja na kupunguza hatari za kupata kansa.
Ingawa duniani kuna zaidi ya aina 3,000 za matunda ya peasi huku kila aina ikiwa na umbo, ladha na virutubisho vya kipekee lakini hapa tutaenda kutumia peasi za rangi ya kijani ambayo inapatikana kwa urahisi katika mazingira yanayotuzunguka.
Kama bado hujui utamu wa kinywaji hiki usijali, leo nitakufundisha ujanja huu ili usiendelee kutumia vinywaji vile vile kila siku.
Mahitaji
Hatua za kufuata
Ili kutengeneza juisi hii anza kwa kuosha peasi zako vizuri kwa kutumia maji masafi na salama ikiwa zimenunuliwa kutoka shambani moja kwa moja ni vyema uzimenye maganda.
Baada ya kuzimenya hatua inayofuata zikate vipande vinne na uondoe sehemu ya katikati yenye mbegu.
Ikiwa unatumia peas za kisasa, unaweza kutumia pamoja na ganda lake hivyo unaweza kuziosha kwa maji ya uvuguvugu.
Hatua inayofuata baada ya kuandaa peasi, weka vipande vyake kwenye blenda na ongeza vikombe viwili vya maji, tangawizi iliyosagwa ikifuatiwa na maji ya limau ili kuongeza ladha zaidi.
Hatua inayofuata katika blenda yenye mchanganyiko anza kusaga juisi kwa dakika 10 hadi 15 hadi mchanganyiko uwe laini, kumbuka kuipumzisha blenda yako na siyo kusaga kwa mfululizo.
Kama juisi ni nzito sana, ongeza maji kiasi na baada ya hapo weka kiminika chako kwenye chujio kisha chuja vizuri ili kuondoa nyuzi za tangawizi ndani yake kama umetumia juicer huna haja ya kuchuja.
Unaweza kuongeza mdalasini, sukari au hiriki kama utapenda lakini hadi hapo, kinywaji chako kipo tayari unaweza kuhifadhi kwenye jokofu au tumia barafu kukipa ubaridi.