Ukwaju ni moja ya matunda yanayosifika kwa kutengenezea juisi. Tunda hili lenye wingi wa Vitamin B, C, K na aina nyingine za madini yenye faida mwilini, linaweza kutengeneza juisi tamu, inayofaa kutumiwa kipindi hiki cha jua kali.
Juisi ya ukwaju haina gharama ukilinganisha na aina nyingine ya juisi. Ina mahitaji machache na inafaa sana kwa watu wenye familia kubwa.
Fuatana nami mpaka mwisho wa makala haya ujifunze na kuongeza ujuzi wa kutengeneza juisi ya ukwaju.
Mahitaji
Maandalizi
Hatua ya kwanza kwenye uandaaji wa juisi hii ukishanunua ni kuuloweka ukwaju kwenye maji kiasi.
Baada ya dakika 10 anza kuukoroga kwa kutumia mwiko, au kijiko kisha bandika jikoni mpaka uchemke.
Ongeza sukari nusu kikombe au zaidi kutegemea na wingi wa juisi yako
Weka vanila robo kijiko, pamoja na hiriki kama utapendelea.
Baada ya dakika tano sukari ikichanganyika vizuri epua na uchuje kisha ache ipoe.
Ikipoa unaweza kuweka kwenye friji ipate ubaridi kidogo au unaweza kuongeza vipande vya barafu na juisi yako itakuwa tayari kwa kunywa.