Huenda umeshawahi kunywa aina nyingi za juisi zenye ladha tofauti na zilizoburudisha koo lako na kukufanya kila mara utamani kujua jinsi zinavyotengenezwa.
Sasa katika orodha yako ya aina ya juisi ulizowahi kunywa ongeza na juisi ya karoti na ndizi itakayokuburudisha huku ikikupa faida lukuki za kiafya.
Juisi ya karoti na ndizi ni kinywaji chenye afya, kitamu na rahisi kuandaa kinachokupa nguvu na virutubisho muhimu katika mwili ikiwepo nyuzi nyuzi na vitamini A zinazosaidia kudhibiti mmeng’enyo wa chakula na afya ya ngozi.
Na kwa kuona umuhimu wa juisi hii leo JikoPoint.co.tz inakusogezea hatua kwa hatua namna ya kuandaa ukiwa nyumbani.
Mahitaji
Hatua kwa hatua namna ya kuandaa
Hatua ya kwanza osha karoti na ndizi kwa maji safi kisha uanze kumenya na kukatakata kwa saizi ndogo itakayoweza kusagika kwa haraka.
Baada ya hapo andaa blenda na uweke karoti kwanza kisha uzisage na maji upate juisi nzito.
Kama unatumia juicer basi unachopaswa kufanya ni kusaga karoti ambazo baada ya hapo utachuja kwa chujio ili kupata juisi nzuri ambayo hutohitaji kusaga.
Hatua nyingine ni kuchukua ndizi na juisi ya karoti kisha kusaga kwa pamoja mchanganyiko huo ambao utatumia dakika 2 mpaka dakika 4 utakuwa umepata juisi tamu na nzito.
Ikiwa unapenda viungo unaweza kuongeza mdalasini wa unga unafaa ingawa sio lazima.
Kama juisi ni nzito ongeza maji au maziwa kidogo hadi upate uzito unaoupenda.
Mpaka hapo juisi yako sasa iko tayari. Unaweza kuihifadhi kwenye jokofu na kunywa bila kuongeza sukari kwani karoti na ndizi tayari zina sukari asilia.