Mambo ya kuzingatia wakati wa kuandaa juisi ya tango

Na Lucy Samson
11 Jun 2022
Hakikisha una blenda, viungo muhimu.  Hutumika kama kinywaji cha kupunguza  uzito na kitambi. Wengi wamezoea tango ni tunda linalotumika zaidi kama kiungo cha mboga, hususani kwenye utayarishaji wa kachumbari na saladi, wengine hulitumia kama pambo la kupambia sahani mezani. Je unajua kama tango huweza kutengeneza juisi tamu yenye faida nyingi mwilini? Hutumiwa kama moja ya […]
article
  • Hakikisha una blenda, viungo muhimu. 
  • Hutumika kama kinywaji cha kupunguza  uzito na kitambi.

Wengi wamezoea tango ni tunda linalotumika zaidi kama kiungo cha mboga, hususani kwenye utayarishaji wa kachumbari na saladi, wengine hulitumia kama pambo la kupambia sahani mezani.

Je unajua kama tango huweza kutengeneza juisi tamu yenye faida nyingi mwilini? Hutumiwa kama moja ya kinywaji cha kusaidia kupunguza uzito na kitambi (slimming juice).

Makala hii ina mengi ya kukujuza kuhusu faida za tango kwenye mwili wa binadamu, pia itakufunza namna ya kuandaa kinywaji hiki chenye ladha ya kipekee.

Kwa mujibu wa jarida la healthline, tango lina faida nyingi kwenye mwili wa binadamu ikiwemo kupunguza uzito na vitambi.

Hii inatokana na ukweli kwamba tango lina asilimia nyingi za maji na nyuzi nyuzi ambazo hurahisisha mmeng’enyo wa chakula. Pia kiwango kidogo za kalori humuondoa mtumiaji kwenye hatari ya kujaza vyakula vingi vya mafuta tumboni.

Tango ambalo hutumiwa zaidi kwenye mlo kama tunda au kuongezwa kwenye kachumbari na saladi huongeza ladha kwenye chakula na linaweza kutumiwa kama mbadala wa vyakula vyenye mafuta.

Tunda hilo husaidia kuufanya mwili kutokuwa mkavu (hydrated) hivyo kuufanya mwili kuwa na nguvu na kupunguza hatari ya kupata choo kigumu (constipation).

Sambamba na faida hizo tango pia linasifika kwa faida zake lukuki kwenye ngozi na nywele ambapo huzipa afya na kuzifanya ziwe na mvuto.

Fuatana nasi uweze kujua namna ya kuandaa juisi ya tango ili kupata faida zake.

Maandalizi

Osha matango kwa maji safi na uyakate kwa vipande vidogo vitakavyoweza kusagika. Fanya hivyo pia kwa tangawizi.

Ukimaliza kamua limao na uchuje tayari kwa ajli ya kuchanganya na juisi yako ikishakuwa tayari

Andaa blenda na uweke vipande vyote kwenye blenda na kikombe viwili vya maji, kisha saga.

Ikishasagika vizuri ongeza mdalasini na usage tena, ikimalizika chuja na uweke kwenye glasi. Ongeza vijiko viwili vya maji ya ndimu, vijiko viwili vya sukari pamoja na vipande vya barafu.

Juisi yako ipo tayari kunywa, unaweza kuweka kwenye friji kwa ajili ya matumizi ya baadae.

© Copyright 2021 JikoPoint by Nukta Africa