Dar es Salaam. Bei ya jumla ya mchele katika jiji la Dar es Salaam imepanda kwa Sh50,000 ndani ya kipindi cha wiki moja, jambo linalowafaidisha wakulima waliopeleka zao hilo jijini humo.
Takwimu za mazao makuu ya chakula zilizotolewa leo (Septemba 23, 2022) na Wizara ya Viwanda na Biashara zinaonyesha kuwa bei ya juu ya gunia la kilo 100 la zao hilo jijini humo ni Sh330,000 katika soko la Temeke.
Bei hiyo imepanda kutoka Sh280,00 iliyorekodiwa Ijumaa ya Septemba 16 mwaka huu.
Kupanda kwa bei hiyo ya juu kutawanufaisha zaidi wafanyabiashara na wakulima huku wanunuzi wakitoboa mifuko yao kwa Sh50,000 zaidi kwa kila gunia moja iwapo hesabu hizo zitapigwa kwa bei ya juu.
Aidha takwimu hizo zinaonyesha kuwa bei ya chini ya zao hilo la chakula inayotumika leo imerekodiwa mkoani Iringa ambapo ni Sh 170,000, ambayo haijabadilika tangu wiki iliyopita.