Hapo vipi? Rosti ya viazi vitamu na kuku choma

Na Lucy Samson
14 Apr 2023
Pishi la viazi vitamu ni rahisi na haichukui muda mrefu hata vijana wa kiume wanaweza kujaribu kupika pishi hili lenye ladha ya kipekee.
article

Kuna aina nyingi za mapishi ya viazi vitamu ila nina uhakika hujawahi kukutana na rosti ya viazi vitamu na kuku wa kuchoma aliyekolea viungo.

Wapishi wengi wa viazi vitamu wamezoea kuvikaanga, kuvichoma au kuvichemsha na kuweka nazi kwa mbali ili kuongeza ladha.

Kutana na Rodgers George, mtaalamu wa mawasiliano atakayekufundisha namna ya kupika rosti ya viazi vitamu pamoja na kuku wa kuchoma kwa kutumia air fryer (mashine ya umeme inayooka kwa mvuke).

Aina hii ya mapishi ya viazi vitamu ni rahisi na haichukui muda mrefu hata vijana wa kiume wanaweza kujaribu kupika pishi hili lenye ladha ya kipekee.

© Copyright 2021 JikoPoint by Nukta Africa