Jinsi ya kupima maji wakati wa kupika wali

Na Maria Acley
19 Jan 2022
Kupima kimo cha maji hauhitaji kujua mambo mengi bali mbinu za kucheza na mwiko wako.
article
  • Unatakiwa uweke mwiko wako kwa mtindo fulani ili kupima maji.
  • Hakikisha kimo cha maji kutoka ulipoishia mchele na ukomo wa maji hakizidi sana mwiko wako.
  • Inashauriwa kutumia maji ya moto wakati wa kupika wali.

Mapishi ya wali ni rahisi kwa wengi lakini kwa baadhi ni magumu. Kinachosumbua zaidi ni kuweka maji yanayotosha kipimo cha kuivisha wali wakati wakupika ili usibaki na kiini au usiwe boko boko.

Unapokuwa jikoni kuoika wali, vitu vinavyosumbua ni upimaji wa viungo au mahitaji muhimu wakati wa kuchanganya vile vikorombwezo vinavyojumuika kutengeneza chakula kitamu chenye viwango.

Kama wewe ni mmoja wa watu wanaosumbuliwa na changamoto hizobasi ondoa shaka. Chukua kiti tukae tuupike huo wali mana Jikopoint ndo sangoma wa mapishi yako.

Mahitaji muhimu ya kupika wali

Kwa kuwa tunapika wali wa kawaida tu, hatuhitaji mambo mengi. Haya ndiyo mahitaji muhimu.

Tuanze kupika “kichele”

Kwa kuanza, chemsha maji kwenye jiko lako la gesi au kama una jagi la kuchemsia maji, chemshia humo.

Osha mchele wako uliochambuliwa vizuri uwe tayari kwa kupikwa. Maji yakipata moto weka chumvi kisha uonje kiasi cha chumvi kwenye maji kama kinatosha. 

Weka mchele wako uliouandaa kwenye mchanganyiko huo wa maji na chumvi kisha koroga kuhakikisha mchele umechanganyika vizuri kwenye maji.

Hatua tunayofuatia ndiyo hatua ambayo huwasumbua wengi. Niombe umakini wako hapo. Ukizngatia hatua hii utasahau kabisa kupika wenye kiini wala bokoboko.

Tupime maji

Anza kwa kuchukua mwiko na kisha weka kwenye sufuria yenye mchanganyiko wako wa maji yenye chumvi pamoja na mchele kama inavyoonekana kwenye picha sehemu A.

Lengo la kuweka mwiko kwenye maji kwa namna hiyo ni kupima kiasi cha maji kitakachotosha kupika wali wetu ukaiva vizuri. Mwiko wako utauweka juu ya mchele uliopo kwenye sufuria.

Baada ya kufanya hivyo hakikisha maji yaloyopo kwenye sufuria yanafika kwenye mwiko kama inavyoonekana kwenye picha upande B. 

Baada ya kujiridhisha kwamba maji kwenye wali yana kipimo hicho, weka mafuta kwenye ya kupikia kiasi cha upawa mmoja kisha ufunikie uweze kuiva.

Baada ya dakika kadhaa,funua chakula chako kwa ajili ya kukitazama maendeleo yake kama maji yamekwisha kauka geuza chakula chako kisha ukifunike tena kwa dakika tano.

Angalia pishi lako na kama wali umelainika, hauna kiini na wala sio bokoboko basi hapo mimi na wewe tutakuwa tumefanikiwa kupika chakula chetu kwa umaridadi haswaa!..

Unataka kujua kupika nini tena? Tuulize kupitia +255 677 088 088.

© Copyright 2021 JikoPoint by Nukta Africa