Pressure cooker ni kifaa muhimu katika maisha ya kisasa, hasa kwa wakazi wa mijini wanaohitaji kupika kwa haraka bila kupoteza virutubisho vya chakula.
Ili kuhakikisha kifaa hiki kinaendelea kufanya kazi kwa ufanisi na kudumu kwa muda mrefu, usafi na uangalifu unahitajika ili kuepuka kujikusanya kwa mabaki ya chakula, harufu mbaya, na hata kuharibika.
Kwa mujibu wa chapisho la mwongozo wa mtumiaji wa jiko hilo lenye la WestPoint, zipo kanuni ambazo unapaswa kuzingatia wakati wa kusafisha..
Leo Jikopoint.co.tz tunakufahamisha hatua kwa hatua za njia ya kusafisha kifaa hiki ili kidumu kwa muda mrefu:
Kabla hujaanza kusafisha, hakikisha pressure cooker umeitoa kwenye plagi ya umeme na uiche kwa muda ili kuondoa joto.
Hatua hii ni ya kiusalama na huepusha ajali zinazoweza kusababishwa na umeme au mvuke uliobaki ndani ya kifaa.
Wakati huo huo, soma mwongozo wa mtumiaji wa kifaa chako kwani kila mtengenezaji anaweza kuwa na maelekezo mahsusi kuhusu usafi na utunzaji.
Baada ya kifaa kupoa, suuza sehemu ya ndani ya sufuria ya kupikia kwa kutumia maji ya uvuguvugu ili kulainisha mabaki ya chakula yaliyoganda na kuondoa harufu.
Hii italifanya sufuria kuwa safi wakati wote na litadumu muda mrefu.
Safisha sehemu ya ndani na nje ya sufuria kwa kutumia sabuni ya vyombo isiyo na asidi kali na sponji laini isiyokwaruza. Epuka kutumia vitu vigumu kama kisu, kijiko au brashi ngumu kutolea uchafu. Matumizi ya vitu hivi yanaharibu uso wa ndani wa sufuria na kuathiri uwezo wake wa kupika sawa sawa.
Kwa madoa sugu, changanya kiasi kidogo cha ‘baking soda’ na maji ya sabuni kisha sugua taratibu mpaka uchafu wote utoke.
Vitu muhimu kama mpira wa kufunga (gasket) na valvu ya kutoa mvuke vinapaswa kutolewa kwa uangalifu na kusafishwa kando kwa kutumia maji ya uvuguvugu yenye sabuni.
Kwa sehemu ambazo ni ngumu kufikiwa, unaweza kutumia brashi laini ili kuhakikisha kila sehemu imesafishwa vizuri.
Mpira ukiachwa na mabaki ya chakula unaweza kupoteza uimara wake na kuvuja wakati wa kupika.
Baada ya kila sehemu kusafishwa kikamilifu, hakikisha unakausha kwa kitambaa kisafi.
Kwa upande wa jiko, iwapo kutakuwa na uchavu tumia kitambaa kufuta na hakikisha unaepuka kutumia maji wakati wa kusafisha ili kuzuia kutu ambazo huenda zikaharibu jiko.
Usihifadhi pressure cooker ikiwa na unyevu kwani hali hiyo huweza kusababisha kutu hasa sehemu za ndani.Baada ya hapo hifadhi kifaa chako mahali pakavu na salama.
Kwa kufuata hatua hizi za msingi utadumisha ubora wa kifaa chako, kuepuka gharama zisizotarajiwa za matengenezo na kuhakikisha chakula chako kinapikwa katika mazingira safi na salama. Kama bado hujamiliki pressure cooker, jikopoint.co.tz inaambaza chapa ya WestPoint kwa bei nafuu. Kwa maelezo, wasiliana nasi kupitia namba 0677088088.