Tofauti kati ya ‘rice cooker’ na ‘pressure cooker’

Na Fatuma Hussein
18 Sept 2025
Ni pamoja na muda unaotumika kupikia na aina za vyakula vinavyopikwa katika vifaa hivyo.
article
  • Ni pamoja na muda unaotumika kupikia na aina za vyakula vinavyopikwa katika vifaa hivyo.

Katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia ya mapishi kuna wa vifaa vingi vya mapishi vinavyotajwa kuokoa muda wa kukaa jikoni kwa kuivisha chakula kwa haraka.

Miongoni mwa vifaa hivyo kuna ‘rice cooker’ na ‘pressure cooker’  ambazo hupika chakula ndani ya muda mfupi.

Ingawa vyote vimeundwa kurahisisha kazi jikoni, matumizi na kanuni zake za utendaji zinatofautiana. 

Ni muhimu kuelewa ipi kati ya vifaa hivi inafaa zaidi kwa mahitaji yako iwe unapika mlo wa mara kwa mara au unapendelea kupika vyakula mbalimbali kwa haraka.

Kwa kuzingatia umuhimu wake, JikoPoint.co.tz  inakuletea kwa undani utofauti uliopo kati ya vifaa hivi viwili.

Rice cooker 

Kwa lugha rahisi, rice cooker ni kifaa cha umeme kilichoundwa mahususi kwa ajili ya kupika vyakula vinavyohitaji mchele.

Utendaji wake ni rahisi na wa moja kwa moja baada ya kuweka mchele, maji na viungo unavyohitaji, kifaa huanza kufanya kazi kiotomatiki.

Ndani yake kuna sensa ya joto (thermostat) inayofuatilia mchakato wa upikaji.

Wakati maji yanapochemka na mchele kuanza kuiva, sensa hupima kiwango cha mvuke.

Mara tu maji yote yanapokuwa yamefyonzwa na mchele kuiva, halijoto ndani ya chombo huongezeka ghafla. 

Sensa hugundua mabadiliko haya na kuzima moto wa kupikia moja kwa moja.

Baadhi ya rice cooker hubadilika kwenda kwenye hali ya ‘keep warm’ (kuweka joto) ili kuhakikisha wali hauungui huku ukiendelea kubaki tayari kwa kuliwa.

Kazi yake kuu ni kukuondolea usumbufu wa kufuatilia sufuria kila wakati na kuhakikisha wali unatoka vizuri kwa usawa.

Kwa upande wa bei, rice cooker hupatikana kwa bei ya wastani wa Sh 45,000 hadi Sh 95,000, kulingana na chapa na ubora.

Pressure Cooker (Jiko la shinikizo)

Kwa upande mwingine, pressure cooker ni kifaa kinachotumia teknolojia ya kisasa zaidi katika kupika.  Kifaa hiki hufungwa kwa nguvu na hakiruhusu mvuke kutoka nje kirahisi.

Kadri chakula kinavyoiva, mvuke hujikusanya ndani na kusababisha shinikizo kubwa (pressure).

Shinikizo hili huongeza kiwango cha joto hali ambayo hufanya vyakula vigumu kama nyama, maharagwe na mbegu nyingine kuiva haraka zaidi.

 Pressure cooker inafaa sana kwa mtu anayependa kupunguza muda wa kupika huku akihitaji kifaa chenye matumizi mengi ikiwemo kupika vyakula vigumu zaidi kama maharage, nyama, supu, makande na hata kuchemsha makongoro.

Kifaa hiki hutumia dakika saba mpaka nane kupika wali tofauti na rice cooker ambayo hutumia muda mrefu kidogo.

Iwapo utatembelea JikoPoint, pressure cooker hasa za West Point hupatikana kati ya Sh17,000 hadi Sh 18,000, kutegemea na aina( manual/ digital)

Hata hivyo, ikiwa lengo lako kuu ni kufanya maisha ya kupika wali pekee kila siku  basi rice cooker ndiyo chaguo bora kwako

Lakini kama unahitaji kifaa chenye matumizi mengi, chenye uwezo wa kupika vyakula kwa muda mfupi, basi pressure cooker ndiyo kifaa sahihi zaidi.

Uamuzi wa kuchagua kati ya rice cooker na pressure cooker hutegemea mtindo wa maisha yako, bajeti yako na urahisi unaoutaka jikoni.

Unapohitaji kumiliki kifaa bora kulingana na hadhi yako, tembelea jikopoint.co.tz au wasiliana nasi kwa simu 0677 088 088.

© Copyright 2021 JikoPoint by Nukta Africa