Fahamu faida kuu tatu za kutumia ‘pressure cooker’

Na Fatuma Hussein
11 Jul 2025
Sio muhimu tena kuuliza ni nani anapaswa kuwa na pressure cooker?
article
  • Inarahisisha kazi, huokoa muda, huhifadhi afya na huleta ladha tamu ya asili.

Katika mazingira ya sasa ambapo mabadiliko ya mtindo wa maisha, hali ya uchumi na uhitaji wa lishe bora unazidi kuongezeka, watu wengi wanatafuta njia mbadala za kuandaa chakula kwa ufanisi na afya.

Pressure cooker (jiko la umeme lenye presha) imeibuka kama suluhisho la kwa changamoto hii katika upishi.

Sio muhimu tena kuuliza ni nani anapaswa kuwa na pressure cooker? bali ni muhimu kujua ‘kwa nini mpaka sasa hutumii pressure cooker?.’

Makala hii inaeleza kwa kina faida tatu za kutumia pressure cooker hasa kwa wapishi wa mboga za majani.

1. Huhifadhi virutubisho zaidi

Moja ya changamoto za upishi wa kawaida ni kupotea kwa virutubisho vinavyohitajika na mwili. 

Watalaam wa afya wanashauri kuwa kupika mboga kwa muda mrefu au kwa maji mengi huondoa virutubisho kama vitamini B, C, pamoja na madini muhimu.

Kupika kwa shinikizo kunatumia muda mfupi na mvuke wenye joto la juu, jambo ambalo huwezesha chakula kuiva haraka bila kuharibu virutubisho. 

Kwa mfano, mboga kama brokoli, karoti au viazi vitamu vinahifadhi kiwango kikubwa zaidi cha virutubisho vinapopikwa kwa shinikizo kuliko kwa kuchemshwa kawaida. 

Haijalishi unapika mboga za majani au mboga tofauti kwa kutumia kifaa hiki virutubisho vya chakula huendelea kubaki pale pale. Picha/ Jiko Point.

Hii ni faida kwa watu wanaojali afya zao, hasa watoto, wazee na wagonjwa wanaohitaji lishe bora.

2. Hupika kwa haraka na huokoa muda

Muda ni rasilimali adimu, pressure cooker inaweza kupika maharage kwa takriban dakika 25 hadi 35 tu badala ya saa 2 kwa mkaa au kuni.  

Hii inamaanisha kuwa unaweza kuandaa mlo kamili kwa chini ya dakika 20, ukiwa na uhakika wa ladha, ubora na usafi.

Pia hupunguza matumizi ya gesi au umeme kwa kiasi kikubwa kwa sababu muda wa kupika hupunguzwa kwa wastani wa asilimia 70.

Kwa kutumia kifaa hiki ambacho unaweza kukipata ndani ya JikoPoint.co.tz unaweza kupika wali na ukaiva chini ya dakika 10 tu. Picha/ Jiko Point.

 Kwa muktadha huu, pressure cooker si tu rafiki wa mpishi mwenye shughuli nyingi, bali pia ni rafiki wa mazingira kwa kupunguza matumizi ya nishati chafu kama kuni na mkaa.

3. Huboresha ladha ya chakula asili

Tofauti na mitindo mingine ya mapishi inayotegemea viungo vikali au mafuta mengi kuongeza ladha, pressure cooker hutumia hali ya joto la juu na mvuke kuhifadhi na kuimarisha ladha asilia ya chakula. 

Maharage hutoka yakiwa laini lakini bado yenye muundo mzuri, na nafaka kama shayiri au mchele huiva vizuri pasipo kuharibika.

Sio chakula asili tu hata kwa kutumia kifaa hiki unaweza kupika ‘chips’ na msosi ukawa mzuri ajabu. Picha/ Jiko Point.

Hii ina maana kuwa unaweza kuandaa mlo wenye ladha ya kuridhisha bila kuongeza viungo vingi visivyo vya lazima, jambo linalowezesha ulaji wa asili, nafuu na wenye afya bora zaidi.

Unasubiri nini kumiliki presha cooker ili kupata faida hizi muhimu?

© Copyright 2021 JikoPoint by Nukta Africa