Faida, jinsi ya kuandaa juisi ya papai na ndizi

Na Mlelwa Kiwale
30 Oct 2024
Kwa wale wanaosumbuliwa na matatizo ya choo kigumu, wagonjwa au watoto wanaoanza kujifunza kula juisi hii ndio yenyewe.
article
  • Kwa wale wanaosumbuliwa na matatizo ya choo kigumu, wagonjwa au watoto wanaoanza kujifunza kula juisi hii ndio yenyewe.

Inawezekana umeshawahi kunywa aina nyingi za juisi zilizoburudisha koo lako na kukupa virutubisho vilivyojenga na kuimarisha afya ya mwili wako.

Sasa katika orodha yako ya aina ya juisi ulizowahi kunywa ongeza na juisi ya papai na ndizi itakayokuburudisha huku ikikupa faida lukuki za kiafya.

Kwa wale wanaosumbuliwa na matatizo ya choo kigumu, wagonjwa au watoto wanaoanza kujifunza kula hii ndio yenyewe.

Maandalizi

Osha papai na ndizi kwa maji safi kisha uanze kumenya na kukatakata kwa saizi ndogo itakayoweza kusagika kwa haraka.

Ukimaliza andaa blenda na uweke mahitaji yako yote pamoja na vipande vya barafu kama unapendelea kisha usage mpaka matunda yote yachanganyike vizuri.

Kama juisi ni nzito sana unaweza kuongeza maji kidogo kidogo au maziwa mpaka upate uzito unaopendelea kisha juisi yako itakuwa tayari kwa kunywa.

Unaweza pia kuichuja lakini kama umeisaga kwa muda mrefu papai na ndizi huwa zinasagika vizuri na hazina nyuzi nyuzi.

Ikiwa hupendelei sukari unaweza usiweke na bado juisi yako ikawa tamu.

© Copyright 2021 JikoPoint by Nukta Africa