Blue Lagoon ni mojawapo ya cocktail zinazopendwa zaidi duniani, ikiwa na sifa adimu ikiwemo rangi samawati angavu inayofanana na bahari safi pamoja na mchanganyiko wa barafu ambao huburudusha wanywaji wake.
Huenda umaarufu wake umetokana na mchanganyiko unaounda kinywaji hicho ambao ni limao, ladha ya machungwa kutoka kwenye kinywaji kingine kinachoitwa ‘Blue Curaçao’ ikisindikizwa na aina mbalimbali ya pombe ikiwemo Vodka.
Kama ulikuwa hufahamu Cocktail ni mchanganyiko wa vinywaji vya pombe na vinywaji vingine kama juisi, sharubati, au matunda hivyo uwepo wake ndiyo unaotoa ladha na maana ya kinywaji tunachokiandaa leo.
Ikiwa wewe ni mtembeleaji wa sehemu za starehe bila shaka umewahi kukutana na kinywaji hiki ambacho bei yake huanzia Sh 18,000 hadi Sh35,000 kwa glasi kutegemeana na sehemu ulipokinunua.
Ili kufurahia utamu wa kinywaji hicho, jiko point imekusogezea maandalizi rahisi ya kukiandaa nyumbani ili uweze kukifurahia pamoja na uwapendao.
Kumbuka kinywaji hiki kinatengenezwa kwa pombe hivyo hakifai kutumiwa na watoto, wajawazito na wagonjwa.
Namna ya kuandaa hatua kwa hatua
Weka kiasi kidogo cha vipande vya barafu (Ice Cubes) katika glasi ikifuatiwa na viipande vya limao (lemon slice) kisha uongeze aina yoyote ya Vodka uipendayo au watakayochagaua wageni wako.
Katika glasi hiyo hiyo mimina Blue Curaçao kiasi mililita 30 ikifuatiwa na soda ya limao na kijiko kimoja cha maji ya limoa ili kuongeza aladha.
haujazi hakikisha unamimina vinywaji hivyo taratibu ili kutengeneza matabaka ya rangi yakayoborhs amuonekano wa kinywaji chako.
Pamba kwa kipande cha limao pamoja na cheri juu ya glasi na baada ya hapo kinywaji chako kitakuwa tayari kwa ajili ya matumizi.
Usikose kuendelea kufuatilia makala zetu kwa maandalizi ya vinywaji vya kuvutia.