Matunda unayoweza kutengenezea juisi ya nanasi

Na Mwandishi Wetu
11 Feb 2022
Faida za juisi ya nanasi ni pamoja na kusaidia mmeng’enyo wa chakula, kusaidia kupunguza uzito na kusaidia tishu pamoja na ngozi kupona haraka. Unaweza kuisaga yenyewe au ukahanganya na matunda mengin.
article
  • Nanasi na karakara ni kwa wanaopenda juizi nyepesi
  • Mchanganyiko wa nanasi na ndizi ni murua kwa wanaopenda vinywaji vizito.
  • Nanasi na maji ya nazi huwapa matokeo mazuri wanaojali ngozi zao na wadau wa mazoezi ya viungo.

Nanasi ni tunda la aina yake. Mbali na kuwa moja ya matunda yanayopatikana kwa takriban mwaka mzima, tunda hili lina faida zake kiafya.

Mtaalamu wa masuala ya lishe Julia Zumpano kupitia tovuti ya Health Essentials, ameandika kuwa, nanasi ni tunda lenye virutubisho mbalimbali ikiwemo vitamini C inayosaidia kupambana na magonjwa ikiwemo saratani na “manganese” ambayo inasaidia katika uundaji wa mifupa.

Faida zigine ni pamoja na kusaidia mmeng’enyo wa chakula, kusaidia kupunguza uzito na kusaidia tishu pamoja na ngozi kupona haraka.

Ili uweze kupata faida zote hizi, unaweza kula nanasi kama lilivyo au ukasaga ili upate juisi. Hata hivyo, wataalamu wa lishe wanashauri kutoichuja juisi hiyo ili mwili wako unufaike na nyuzi nyuzi za tunda hilo.

Kama hauwezi kunywa juisi ya nanasi peke yake na ungependelea kuchanganya na matunda mengine, haya ni baadhi ya matunda unayoweza kutumia ili ufurahie juisi yako.

Juisi ya nanasi inaweza kuchanganywa na matunda mengine ikiwemo karakara, maji ya nazi na embe. Picha| The Mercury News.

Nanasi na karakara (pesheni)

Hii ni kwa wanaofurahia vinywaji vyepesi na ambavyo vina uchachu kwa mbali.

Unachohitaji ni nanasi ambalo limeiva vizuri na karakara mbili za saizi ya wastani. 

Menya nanasi kisha kata vipande vidogo vidogo na weka kwenye blenda. Kata karakara kisha weka tunda zake kwenye kikombe tofauti kama hautotaka kuchuuja juisi yako.

Anza kusaga nanasi weka kwenye jagi na kisha saga karakara na uchuuje juisi ya karakara pekee na uichanganye na ile ya nanasi ambayo haijachujwa.

Kama utachuja juisi yako ya nanasi, changanya matunda yote kwenye blenda na usage kwa pamoja.

Uchachu wa karakara na utamu wa naansi ni pepo duniani. 

Nanasi na ndizi

Mchanganyiko wa nanasi na karakara ni wa aina yake. Picha| Laylita.

Katika ununuzi wa nanasi, unaweza kupata nanasi chachu ambalo litakulazimu uweke sukari ili upate juisi tamu. Huenda ulikuwa haujafikiria kutumia sukari mbadala, sukari ya ndizi inaweza kukufaa.

Mchanganyiko wa nanasi na ndizi ni wa aina yake.

Siyo lazima nanasi liwe chachu. Hata likiwa tamu bado unaweza kutengeneza juisi hii. 

Tovuti ya masuala ya chakula, Food Pairing mapendekezo nanasi na ndizi kama moja ya mchanganyiko unaweza kuupenda. 

Wakati nanasi ikikupatia nyuzi nyuzi, ndizi huchochea usingizi, husaidia kinga ya mwili na pia inatajwa kupunguza msongo wa mawazo.

Nanasi na maji ya nazi (dafu)

Faida za naansi na maji ya nazi ni lukuki. Usikubali zikupite. Picha| Food and wine magazine.

Baadhi ya watu hupata ugumu kunywa maji ya nazi. Kwa mujibu wa Opera News, juisi ya nanasi na maji ya nazi ina faida nyingi ikiwemo kuongeza nguvu kwa wanaofanya mazoezi na kuchochea mmeng’enyo wa chakula.

Pia, juisi hii inasaidia kuchochea mlinganyo wa hisia (mood) huku kwa wanaopenda ngozi zao, ikiwapatia mng’aro wa aina yake.

Una sababu gani ya kutonunua nanasi lako la buku na nazi ya 500 walau mara mbili kwa wiki?

Nanasi pia huendana na parachichi, tufaa na embe. 

Endelea kusoma JikoNews kwa madini ya afya yako.

© Copyright 2021 JikoPoint by Nukta Africa